KATIKA hali ya kushangaza, mwalimu wa kiume katika shule ya msingi
Chididimo Kata ya Zuzu katika Manispaa ya Dodoma (jina tunalo), juzi alitinga mkutanoni akiwa amevalia sketi
na blauzi ya kitenge huku akiwa amesuka nywele za bandia na kuzua gumzo
mkutanoni hapo.
Licha ya mwalimu huyo kuvaa viatu vya kiume na soksi fupi, alikuwa
akitembea mwendo wa kiume huku mikanda ya sidiria aliyokuwa ameivaa kujitokeza
mara kwa mara.
Haya yalitokea katika kijiji cha Chididimo wakati wa Wiki ya Maji
kimkoa, ambapo pamoja na mambo mengine kulikuwa na uzinduzi wa mradi wa maji.
Mwalimu huyo alikuwa kati ya wacheza ngoma wa kikundi cha Mpango
Kazi Chididimo, lakini ilikuwa ni vigumu watu wasiomfahamu kumtambua. Hata
hivyo watu walianza kupata wasiwasi kuwa hakuwa mwanamke wakati kikundi hicho
kilipoingia uwanjani, ambapo alikuwa akiimba kwa sauti nzito.
Lakini, maswali ya wageni waliohudhuria mkutano huo, yalipata
majibu mara baada ya mwalimu huyo kupanda jukwaani akiwa na mwenzake kwa ajili
ya kuimba shairi.
Kutokana na hilo ndipo wanakijiji walipoanza kutoa siri kuwa
alikuwa ni mwanaume na ni mwalimu wa shule ya msingi kijijini hapo.
Kutokana na utata na minong’ono iliyosambaa mkutanoni hapo, mwongozaji wa sherehe hizo alimfuata mwalimu
huyo na kuzungumza naye kwa muda na aliporudi alikuwa tayari na jina la mwalimu
huyo na kusema kuwa mwenye nywele ndefu ameshalifahamu jina lake kisha
kulitaja.
Mshereheshaji huyo alisema hata
nyimbo na shairi ambalo wanafunzi waliimba, alitunga mwalimu huyo ambaye
ni mahiri katika sanaa.
Mwalimu huyo alikiri kuwa sanaa ipo kwenye damu yake na alifanya
hivyo kama msanii.
0 comments:
Post a Comment