Mratibu wa
michezo ya Bahati Nasibu kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania Bakari Maggidi
(kushoto) akiangalia majina ya watu waliokuwa wakishindanishwa katika bahati
nasibu ya Ascend Y200 iliyochezeshwa na Tigo, katikati ni Meneja wa Bidhaa wa
Tigo William Mpinga na kulia ni ofisa kutoka Tigo David Semkwao (Picha na Mpiga
Picha Wetu)
Na Mwandishi
Wetu
MWANAFUNZI
wa Chuo Kikuu
Kishiriki
Cha Afya cha mkoani Kilimanjaro (KCMC) Fredy Mgaya ni mmoja kati ya washindi
wawili walioshinda bahati nasibu ya Ascend Y200 iiliendeshwa inayoendeshwa na
kampuni ya simu ya mkononi ya Tigo.
Mwingine aliyeshinda
ni David Semkwao ambae ni msanifu wa majengo mkazi wa Ubungo ambapo washindi
wote hao wanapata nafasi ya kuelekea nchini jijini Beijing nchini China kwa
matembezi.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana baada ya kuchezesha bahati nasibu hiyo, Meneja wa
Bidhaa wa Tigo, William Mpinga alisema kuwa washindi hao watalipiwa gharama
zote kuanzia tiketi za ndege, maradhi na fedha za kujikimu wakiwa chnini humo.
Alisema kuwa
wakiwa nchini China watatembelea vivutio mbalimbali vya utalii kama vile ukuta
wa Beijing na maeneo mengine muhimu.
Alifafanua
kuwa Tigo inaendelea na kampeni yake bahati nasibu hiyo ambayo ni maalum kwa
wateja watakaonunua simu aina ya Ascend Y200.
Wakizungumzia
ushindi huo washindi walioshinda bahati nasibu hiyo ya jana waliwasihi watu
wengine nao kujitokeza kununua simu hizo ili waweze kushinda bahati nasibu
hizo.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment