WALIMU 529 wamefukuzwa kazi katika miaka mitatu iliyopita kutokana na utoro
maeneo yao ya kazi.
Katibu Msaidizi, Idara ya Utumishi wa Walimu
katika ofisi ya Tume ya Utumishi wa Umma, Christina Hape alisema idadi hiyo
inatokana na mashauri 669 yaliyofikishwa kwenye ofisi zao kutokana na utoro wa
walimu kwa zaidi ya siku tano.
Alisema mwaka 2010/2011 walipokea mashauri 260,
mwaka 2011/12 mashauri 152 na mwaka 2012/13 mashauri 257.
“ Hayo ni mashauri ambayo yamefika makao makuu,
na baadhi yake yalirejeshwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na
kukosewa taratibu. Lakini katika ngazi ya wilaya zote nchini mashauri 1,128
yalishughulikiwa,” alisema.
Alisema ni makosa kwa walimu kuwa nje ya kituo
cha kazi bila kufuata taratibu na kuwa suala hilo linakwenda pia kwa walimu wa
serikali wanaofundisha masomo ya ziada kwenye shule binafsi wakati wa muda wa
kazi.
Kuhusu makosa ya walimu wenye uhusiano wa
kimapenzi na wanafunzi, Hape alisema walimu 84 walikutwa na kosa hilo kuanzia
mwaka 2008 hadi 2012 na kukiri kuwa tatizo hilo ambalo linachangiwa na
wahusika, jamii kushindwa kutoa ushahidi ili kuwatia hatiani walimu waliofuata
maadili ya kazi zao.
Akizungumzia walimu walioripoti vituo vya kazi
katika ajira za mwaka jana, Katibu Msaidizi
katika idara hiyo, Evelyne Omari alisema walimu 11,000 walisajiliwa
baada ya kusaini mkataba na mwajili wao na kukiri kuwapo baadhi ya walimu ambao
wamekuwa hawajisajili kwenye tume hiyo.
Naibu Katibu Mkuu, Edwin Mikongoti alisema tume yake imekasimisha madaraka kwa
wakuu wa shule, vyuo na walimu wakuu kushughulikia makosa ya madogomadogo ya
kinidhamu na kutoa adhabu kwa walimu na wakufunzi.
0 comments:
Post a Comment