Famous Comedian in town who was the Master of Ceremony, Evance Bukuku (left) Coca - Cola Brand Manager Maurice Njowoka, Lady Jaydee and Evance from this blog |
Njowoka insists something to Jide |
Madee |
The B Band |
Diamond the Coca Cola's ambossodor |
Country Director for Coca-Cola
Tanzania, Yebeltal Getachew (left ) Diamond and Coca Cola brand Manager in Tanzania Maurice Njowoka
|
Some hugs |
Ongeza kichwa |
Na Evance
Ng'ingo
KWA sasa
katika medani ya muziki hapa nchini na duniani kote kumekuwa harakati zinazofanywa na wadau mbalimbali wa
muziki ambapo wameamua kuwekeza katika fani hiyo.
Uwekezaji
huo katika muziki upo kwa aina mbalimbali ambapo wapo ambao wanawekeza kwa
kuwasaidia wasanii kujiinua kimuziki na pia wao ambao wanajipanga kuwekeza kwa
kufungua miradi kadhaa ya kukuza muziki.
Miradi hiyo
ni kama vile ile ya kuwekeza studio au vifaa vingine vya muziki ambapo wasanii
wanaendelezwa kisanaa.
Miradi kama
vile Tusker Project Fame, Epiq Bongo Star Search au ile iliyokuwa CocoCola Pop
Idol ni moja kati ya miradi ambayo makampuni makubwa yamewekeza au kudhamini
kwa lengo la kusaidia sanaa.
Miradi
mingine inalenga kuinua asili ya muziki kwa kuanzisha nyimbo zenye vionjo vya
muziki wa asili.
Mradi wa Coke
Studio ni moja kati ya miradi ya kuendeleza muziki hapa nchini wenye lengo la
kuendeleza muziki wa kisasa wenye asili ya Afrika.
Coke Studio
ni kipindi muziki ambacho kitakuwa kikirushwa kwenye runinga na kwa hapa nchini
kwa kuanzisha kitahusisha wasanii kama vile Nasib Abdul, Diamond na Judith
Wambura, Lady Jaydee.
Hicho ni
kipindi ambacho kitahusisha wasanii wenye miondoko tofautitofauti ya kisasa
kitakuwa kikiitwa Coke Studio Afrika.
Kipindi
hicho kinahusisha wasanii kutoka Afrika Mashariki na wengine wa kutokea Afrika
Magharibi na Kusini.
Wasanii
kutoka kona nyingine ya Afrika ni pamoja na Seif Keita kutoka nchini Mali, King
Sunny Ade, Mi, Waje, Jimmy Jat and Bez froma Nigeria.
Kwa upande
wa Afrika Mashariki wengine ni pamoja na
Octopizzo, Miss Karun and Just a Band wakiwa wanatokea nchini Kenya na pia kuna
Hip Hop Panstula pia kuna na Lilian Mbabazi
wa Uganda pia.
Pia wapo
akina Boddhi Satva pamoja na Tumi wa Afrika Kusini pamoja na kundi la Culture
Music la kisiwani Zanzibar.
Kitaanza
kurushwa kesho kuanzia saa tatu usiki katika luning ya ITV ambapo kitaanza
kuoneshwa kwa miezi miwili.
Wasanii hao
akina Diamond na Lady Jaydee ni wasanii ambao walienda nchini Kenya kwa ajili
ya kushiriki katika kurekodi kipindi hicho.
Baada ya
kumalizika kwa season one ndio itaanza rekodi ya season 2 ambapo wasanii
wengine watachaguliwa pia.
Umoja wa
wasanii mbalimbali kama hao wakishiriki kwenye kipindi hicho watasaidia
harakati za kupata muziki wa kisasa wenye asili ya Afrika.
Pia kutakuwa
na wasanii walioshirikishwa katika kipindi hicho ambapo kutakuwa na wasanii kama vile Bamboo wa
Kenya, Sega na Dela pamoja na Kassongo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na
pia Temi Dollface kutoka Nigeria.
Akizungumza na
waandishi wa habari Meneja wa Bidhaa wa Coca-Cola Tanzania Maurice Njowoka
anafafanua kuwa Coke Studio itakuwa ikioneshwa Kenya, Uganda, Tanzania na
Nigeria.
Anaongeza
kuwa itaenda hewani kwa vipindi vinane vya dakika 45 kila kimoja huku kukiwa na
saa mbili za vipindi maalum kwa mwaka mpya.
Aliongeza
kuwa katika kila kipindi kutakuwa na masuala mbalimbali muhimu katika sanaa
ambapo anatolea mfano wa ujengaji wa sauti za kipekee kutoka kwa wasanii.
" Pia
kutakuwa na fursa ya watazamaji kuona kile kitakachokuwa kikijili nyuma ya
pazia ambapo wataona namna kipindi kinavyotengezwa na mengine" alisema
Njowoka.
" Kwa
ni fursa kubwa sana kwa Tanzania kushirikishwa kwenye kipindi kama hiki kwa
kuwa kuna nchi nyingi Tanzania ambazo zingependa kuwa na miradi kama hii lakini
kwa sasa ni Tanzania ipo na wasanii wetu
pia wamo." alisema Njowoka.
Anaongeza
kuwa hiyo ni fursa kubwa kwa wasanii wa
hapa nchini kutangaza kazi zao za sanaa pamoja na kuonesha vipaji vyao katika
nchi nyingine nyingi za Afrika.
Anatolea mfano
kwa nchi kama Pakistani ambao kipindi hicho kimekuwa na mafanikio makubwa huku
kikikadiriwa kuwa na watazamajimilioni 77 kwenye You Tube peke yake.
Akizungumzia
ushiriki wake katika kipindi hicho msanii Lady Jaydee anasema kuwa amekuwa
akiimba na kujitangaza sehemu mbalimbali za ndani na nje ya Tanzania.
Anasema kuwa
anaona kuwa kipindi hicho kitasaidia kuinua harakati zake za kujitangaza zaidi
nje ya nchi.
"Kupitia
kipindi hiki sisi kama wasanii mbali na kukuza vipaji vyetu, kukutana na
kufanya kazi pamoja na wasani wengine lakini pia ni wakati muafaka kusema kwa ile ndoto yangu ya kujitangaza
kimataifa zaidi inaenda kukamilika"
alisema Lady Jaydee.
Kwa upande
wake msanii Diamond Platnumz anasema kuwa akiwa kama balozi wa Coca Cola hiyo
kwake ni muendelezo wa fursa ambazo amekuwa akizipata kupitia kampuni hiyo.
Kipindi
hicho asili yake ni nchini Brazil ambapo kimekuwa kikiitwa Estudio Coca - Cola
ambacho kilirushwa kwa mara ya kwanza machi 2007.
Kikiwa
kinaoneshwa hapa nchini washabiki watakuwa na fursa ya kuona na pia kupakua
(downloading) vitu mbalimbali kama Video huku pia wakiwa katika nafasi ya
kushinda vitu mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment