Kulikuwa na burudani safi |
Meneja wa Masuala ya Kijamii wa kampuni ya Tigo, Woinde Shisael akizungumza na waandishi kuhusiana na ushiriki wa Tigo katika kampeni hiyo |
Pia kulikuwa na Fashion Show |
Mkurugenzi Mtendaji wa Bonah Trust Fund, Bonah Kalua |
Kikundi cha Sanaa cha Safi Cultural Center |
Mwanamitindo Mahiri Asia alikuwapo kusaidia kutoa burudani |
Picha ya pamoja kati ya Bonah Kalua na wageni waalikwa |
Mimi niliamua kuchangia pia ili kufanikisha harakati za mwanamama Bonah Kalua (kushoto) ambae ni Diwani wa Kipawa |
Pia kwa pamoja tunaweza kusaidia harakati hizo za Bonah pamoja na Tigo kwa kuchangia.0716 667470 |
Haya Habari Kamili
Kwa sasa wadau mbalimbali wanazidi kujitokeza katika kusaidia harakati za serikali za kuimarisha elimu hapa nchini.
Tumeshuhudia Tasisi ya Hassan Majar Trust Fund ambayo hivi majuzi imezindua harakati zake za kusaidia upatikanaji wa madawari nchini kwa ajili ya kusaidia wanafunzi kusoma wakiwa wanatumia madawati.
Pia wapo wadau wengine mbalimbali kama vile Mamlaka ya Elimu Tanzania ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa ikisaidia ujenzi wa mabweni kwa kusaidiana na wadau mbalimbali wa maendeleo nchini.
Hivi majuzi ilizinduliwa rasmi Taasisi inayojishughulisha na kusaidia uboreshaji wa elimu ya Bonah Education Trust
Fund na ilianza kampeni ya kuchangisha fedha za kulipia ada
wanafunzi.
Taasisi
hiyo ilizinduliwa katika Uwanja cha Mnazi Mmoja na Meya wa Manispaa ya Ilala
Jerry Slaa jana ambae aliwataka wananchi kuchangia fedha kwa lengo la kuwalipia
ada wanafunzi 100 wa sekondari.
Slaa
alisema kuwa ili kuwa na jamii bora inatakiwa vijana wapate elimu na kuongeza
kuwa elimu ya sekondari ni msingi mzuri wa utakaowawezesha watoto kuona mbali.
Alisema
kuwa mbali na serikali kuwa na kampeni ya kusaidia ujenzi wa mabweni, madarasa
na vyumba vya maabra ni muda wa wanajamii kuhakikisha kuwa mabweni hayo na
madarasa hayo yanatumiwa na wanafunzi.
"
Najua hata tukijenga madarasa na mabweni kama hakuna wanafunzi ni kazi bura
kabisa kinachotakiwa ni wanafunzi kupelekwa shule na ili kufanikisha hilo ni
lazima kuchangia hivyo basi chondechonde tuungane"alisema Slaa.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Bonah Kalua ambae pia ni Diwani wa Kata ya
Kipawa, alisema kuwa kutakuwa na kampeni mbalimbali za kuwataka wanajamii
kujitokeza na kuchangia.
Alisema
kuwa kuna namba ya simu ambayo ni 0716 667470 ambapo walioguswa na harakati
hizo wanaweza kuchangia kwa njia ya Tigo pesa
Kwa
upande wake Meneja anaeshughulikia masuala ya Huduma za Kijamii wa Tigo, Woinde
Shisael alisema kuwa Tigo inaendelea na harakati za kuwarudishia wanajamii
mafanikio yake kwa kusaidia masuala ya elimu na mengineo.
"
Tigo ina furaha kubwa kusaidiana na Taasisi hii katika kuifikia jamii ya
kitanzania na kuipatia elimu na tuna imani kuwa fedha zinazochangiwa
zitasaidia wanafunzi hao kupata elimu
bora" alisema Woinde.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment