Help Children
Love them
Saidia Watoto

Sunday, February 24, 2013

Tume ya kuchunguza matokeo form 4 yaundwa






hatimaye imeonesha usikivu kwa kukubali maoni ya wadau mbalimbali wa elimu nchini na kuunda Tume Maalumu itakayochunguza matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne.
Matokeo hayo yaliyotangazwa Februari 18 na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, yalionesha watahiniwa asilimia 60 kufeli mtihani huo uliofanywa Oktoba mwaka jana, na kuzua maswali kwa wadau.
Baada ya wadau hao wakiwamo viongozi wa vyama vya siasa na Serikali kupendekeza kuchukuliwa hatua kuhusiana na matokeo hayo mabaya kupata kutokea katika historia ya elimu nchini, Serikali imeridhia na kuitikia mwito huo.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lyimo katika taarifa yake jana, alisema Tume hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kazi wakati wowote wiki ijayo, inajumuisha wadau kutoka Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi (TAMONGSCO), taasisi za dini zinazotoa huduma ya elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Asasi Zisizo za Serikali (AZISE) zinazoshughulikia elimu. 


Wadau wengine watatoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA).

Aliwaomba wadau wa elimu, wazazi, walezi na wananchi kwa ujumla wao watoe ushirikiano kwa Tume ili iweze kufanya kazi yake kwa ufanisi.

Hata hivyo, Lyimo katika taarifa yake fupi, hakutaja majina ya watakaounda Tume hiyo wala muda itakayopewa kukamilisha kazi yake.
Matokeo
Akitangaza matokeo, Dk Kawambwa alisema zaidi ya nusu ya wanafunzi waliofanya mtihani
wa Taifa wa Kidato cha Nne, wamepata daraja sifuri na kufafanua, kwamba kati ya wanafunzi
397, 136 waliofanya mtihani huo, 240,903, ndio waliopata daraja sifuri.

Alisema waliopata daraja la kwanza ni 1,641, la pili 6,453 na la tatu 15,426 na kuongeza kuwa wanafunzi 24 ambao matokeo yao yalifutwa kwa kuandika matusi kwenye masomo mbalimbali wakionesha utovu wa nidhamu wa hali ya juu na kwamba Serikali haitavumilia.

“Tunaangalia hatua za kisheria za kuchukua dhidi yao.  Na kwa wale waliofanya udanganyifu wanaweza


 
“Ukiangalia zilizofanya vibaya, ni zenye changamoto ya kukosa walimu hususan wa Sayansi
na Hisabati, kutokuwapo kwa maabara za shule na upungufu mkubwa wa vitabu vya kiada na ziada na kuwa na uwiano wa kitabu kimoja kwa wanafunzi 10,” alisema.
Iundwe Tume
Baada ya kutangaza matokeo hayo, chama cha NCCR-Mageuzi kupitia Mwenyekiti wake, James Mbatia, kilimwomba Rais Jakaya Kikwete aunde Tume itakayojumuisha wataalamu waliobobea katika elimu ili kupata suluhu ya kuendelea kushuka kwa elimu, kwa kuwa limekuwa janga la kitaifa.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa naye alipendekeza iundwe Tume kuchunguza hali hiyo ya idadi kubwa ya wanafunzi kufeli mtihani huo.
 “Matokeo ya Kidato cha Nne yamenisikitisha sana maana asilimia 60 ya wanafunzi kupata sifuri ni jambo la hatari. Napenda kumsihi Rais Kikwete, amefanikiwa katika sekta nyingine kama barabara… aunde tume kuchunguza sababu za wanafunzi kufeli, lakini kubwa kuliko zote tume hiyo ije na mapendekezo ya namna bora ya kuboresha mfumo wetu wa elimu,” alisema Lowassa.
Alisisitiza kuwa hoja ya kutaka Serikali iunde tume kuboresha mfumo wa elimu, alipata kuitoa mara kadhaa kwani anaamini katika kaulimbiu ya ‘Elimu Kabla, Kilimo Kwanza’.
“Kila Mtanzania anasema lake, wengine wanasema ni hujuma, wengine wanadai kuna mgomo baridi wa elimu, malalamiko na sababu ni nyingi na njia pekee ya kujua ukweli ni kupitia tume,” alipendekeza Lowassa.
Kurudia mtihani
Wakati hayo yakiendelea, Serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo imesema inaangalia utaratibu wa watahiniwa waliopata daraja sifuri kurudia mtihani mwaka huu kwa gharama zake.
Aidha, ikasema matokeo hayo mabaya yamesababishwa na mambo makuu manane; kubwa likiwa ni wanafunzi kupita bila kuchujwa katika mtihani wa Kidato cha Pili walioufanya miaka miwili
iliyopita.

Ingawa hata hadidu za rejea kwa tume hiyo hazikutajwa jana, pengine zikisubiri izinduliwe rasmi, ni dhahiri pamoja na mambo mengine, itachunguza pia chanzo cha watahiniwa badala ya kujibu maswali, wamekuwa wakiandika matusi na kuchora vibonzo.

Pia itaweza kuchunguza utendaji kazi wa walimu na kuhusiana na migomo, lakini hasa kutafuta suluhu ya nini kifanyike kuhakikisha wanafundisha katika mazingira mazuri, huku wanafunzi nao wakijibidiisha katika masomo yao.

Suala la uwiano wa walimu na wanafunzi, pamoja na vifaa vya kufundishia na kujifunzia na maabara, huenda nalo likawamo hususan katika shule za sekondari ambazo nazo zimezua mvutano miongoni mwa wadau kuhusu hoja ya kujengwa bila maandalizi ya kutosha.
mwisho

0 comments:

Post a Comment