WATU watatu
wakazi wa kitongoji cha Mkoe kijijini Miangalua wilayani
Sumbawanga wamekamatwa na kuhojiwa na Polisi Mkoa wa Rukwa
wakituhumiwa
kuhusika na kisa
cha kumnyofoa mlemavu wa ngozi ,
Maria Chambanenge
(39) na kutokomea nao
.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi
jana katika kitongoji hicho cha
Mkoe kijijini Miangalua , Diwani wa Kata ya Miangalua , Semakweli Sindani
amethibitisha kukamatwa kwa
watuhumiwa hao ambapo amewataja
wawili
kati yao akiwemo
mume wa mwanamke
huyo mlemavu wa ngozi aitwaye
Gabriel Yohana (43) na
mdogo wake Gaudensi Yohana .
Hata hivyo diwani
huo hakuweza kutoa taarifa zaidi
huku akieleza kuwa
watuhumiwa hao ni
miongoni mwa genge la majambazi
ambao kabla ya
kumtendea unyama
huo mwanamke huyo albino siku chache kabla wanadaiwa
kuvamia nyumba
moja kijijini Ilamba , Kata ya
Kipeta wilayani humo
ambapo walimteka kijana mmoja mlemavu wa ngozi
ambaye jina lake
halikuweza
kufahamika mara moja ambapo ‘kimuujiza’
alifanikiwa
kuwaponyoka na
kurejea kijijini humo.
Hata hivyo wake wenza wa Maria waitwao Honoratha Xevia
maarufu mama
Daria na mwenzake Estha Pesambili maarufu kama mama Ray wamedai mgeni
aliyefikia nyumbani kwao
na kuishi hapo waliyemtaja kwa
jina moja la
Sirukala kuwa
amekamatwa….
Wakimweleza mwandishi
wa habari hizi walidai kuwa
wao wanafahamu kuwa
mume wao Gabriel yupo mjini
akimuuguza mke mwenzao Maria
ambaye bado
amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini
Sumbawanga
“Huyu mgeni ,
Sirukala yeye tulikuwa tukiishi
naye nyumbani akisaidia
kupalilia mashamba
yetu hapa siku hiyo
ya tukio saa 10 jioni aliondoka
nyumbani hapa
bila ya kutuaga hadi leo
bado hajarudi hadi tulipopata
taarifa kuwa
amekatwa akihojiwa na pilisi mjini
Sumbawanga .
Sisi tunachofahamu
ni kwamba mume
wetu bado yupo
hospitalini mjini
Sumbawanga akimuuguza
mke mwenzetu ambaye amelazwa huku …alisema mama
Ray
.
Habari ambazo pia zimethibitishwa na baadhi ya wakazi wa
kitongoji hicho
cha Mkoe kijijini Miangalua akiwemo Diwani wa Kata hiyo ya
Miangalua (CCM)
, Sindani.
Hata hivyo habari za kipolisi licha ya kukiri kukamatwa kwa
watuhumiwa hao
watatu lakini
mtoaji taarifa wake amekataa
kutaja majina yao kwa
kigezo kuwa bado
upelelezi unaendelea ili
kuwabaini wengine “Ofisa wa
Upelelezi wa Mkoa wa
Rukwa , (Peter Ngusa) bado yuko
eneo la tukio
akiongoza msako huko ….. kwanza wewe nani
kakupatia habari hizi akiwa
tayari atakutaarifu
kwa sasa ni mapema mno “ alisema mtoa habari wa polisi
kwa masharti ya
kutoandikwa jina lake gazetini.
Hata hivyi
jitihada za mwandishi wa habari hizi
kumpata Ngusa katika
simu yake ya
mkononi ziligonga ukuta kwani
ilikuwa haipatikani .
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga , Mathew Sadoyeka
akiongozana na wajumbe
wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa
wilaya hiyo kutembelea
nyumba
alimofanyiwa unyama
huo Maria katika kitongoji cha Mkoe
alielezwa
na Mkaguzi Msaidizi
wa Polisi Luka Mwampamba kwamba mama huyo alifanyiwa
unyama huo huku mtoto wake mkubwa wa kike
aitwaye Shukuru (7)
anayesoma Darasa la
Kwanza akishuhudia .
Inadaiwa mama huyo
mlemavu wa ngozi ambaye
ana watoto wanne wote
si albino alikuwa akimnyonyesha mtoto wake mchanga
wa miezi miwili .
Akizungumzia tukio hilo juzi , Gabriel ambaye ni
mume wa Maria wakati
akimuuguza mkewe huyo katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa
mjini hapa ambapo
amelazwa kwa
matibabu alidai watu hao wakiwa
hawafahamiki idadi,
walivamia nyumba yao usiku wa manane wakati mkewe akiwa
amelala na watoto.
Alidai kuwa kabla ya kufanya unyama huo, watu hao walifunga
milango ya
nyumba zote kijijini hapo kwa kamba.
Kwa mujibu wa madai ya Gabriel, Mariamu ni mkewe mdogo, ana
watoto wanne na
usiku wa tukio, alikuwa amelala kwa mke mkubwa aitwaye
Honoratha .
Alidai kuwa baada ya wavamizi hao kufanya unyama huo, mtoto
mdogo wa kaka
yake, alimwamsha akimwambia kusikia kelele kutoka nyumba ya
mke mdogo.
“Ndipo nilipokurupuka kwenda huko, lakini nilikuta milango
yote imefungwa
kwa nje kwa kamba ya katani na dirisha limevunjwa na watoto
na mama yao
wakiwa wanalia.
“Tulipofungua mlango na kuingia ndani, nilimkuta mke wangu
akiwa
anagaragara sakafuni kwenye dimbwi la damu kwa maumivu, huku
mkono wake wa
kushoto ukiwa umekatwa na watu wasiofahamika na kutokomea
nao
kusikojulikana,“ alisema.
Gabriel, ambaye alimsindikiza mkewe hadi hospitali ya mkoa
wa Rukwa mjini
Sumbawanga ambapo amelazwa kwa matibabu, alidai kuwa kabla
ya kumfikisha
hapo, mkewe huyo alipewa huduma ya kwanza katika zahanati
katika mji mdogo
wa Laela, wilayani Sumbawanga.
Alisema walilazimika kupata huduma ya kwanza kwa kuwa Maria
alikuwa na
majeraha makubwa kichwani, baada ya kukatwa na panga na watu
hao
wasiofahamika.
Habari za kipolisi
zimeleza kuwa watuhumiwa hao
watafikishwa mahakamani
mara tu upelelezi
wa awali wsa shauri lao utakapo kamilika huku msako
mkali ukiendelea
kuwabaini wengine ambao
wanadai walifanikiwa kutoroka
na kujificha kusikojulikana .
wakati huohuo, MKAZI
wa kijiji cha Miangalua wilayani
Sumbawanga , Bernad Chambanenge
(79) ambaye
ni baba mzazi wa mwanamke
mwenye ulemavu wa ngozi, Maria
Chambanenge (39), mkazi wa kitongoji cha Mkoe amelaaani na kusikitishwa
na unyama aliofanyiwa
binti yake huyo kwa kunyofolewa
mkono wake wa
kushoto na watu
wasiofahamika kisha kutokomea nao .
A kiwa na uso wa
huzuni huku kijijini Miangalua jana
alimweleza
mwandishi wa
habari hizi kuwa kisa hicho
cha kikatili
alichofanyiwa binti yake
huyo hivi karibuni kimewatia
hofu kubwa
wanawe wengine
ambao nao pia
ni walemavu wa
ngozi wanaoishi
kijijini humo .
Kwa mujibu wake mkewe
aitwaye Ezenia Mtavya (70) amemzaliwa watoto 12
ambapo sita miongoni mwao ni
walemavu wa ngozi
miongoni mwao walio
hai kwa sasa ni wanne
baada ya wawili kufariki dunia .
“Mie na mke wangu
hatujawahi kuwanyanyapaa watoto
hawa ambao ni
albino
kwani wote tumewalelea
sawa sawa bila ubaguzi wa aina
yeyote
isitoshe Maria ni kipenzi
changu …….. kwa sasa naishi
na
kitindamimba aitwaye
Zaina ambaye pia
ni albino
Hivyo kutokana na
usalama wa wanangu hawa kuwa hatarini
naomba
Serikali
iwapatie ulinzi wa kutosha” alisema
Akisimulia kisa cha
binti yake huyo kunyofolewz mkono wake wa kushoto
alidai kuwa usiku
huo wa mananbe akiwa amelala nyumbani
kwake katika
kitongoji cha
Mkoe kijijini Miangalua na
watoto wake wawili ambao
si
albino akiwa anamnyoyesha mtoto wake
wa miezi miwili watu
wasiofahamika
waliingia ndani ya nyumba hiyo
wakipitia dirishani na
kumyofoa mkono wake wa kushoto wakitumia panga .
Alidai kuwa wakati
unyama huo ukifanyika,
mtoto wa mlemavu huyo
wa
ngozi wa kike mwenye
umri wa miaka saba anayesoma
Darasa la Kwanza ,
aitwaye Shukuru
aliyekuwa amelala chumbani na mama yake
alishuhudia
majambazi hao
walikuwa na panga wakiushika
mkono huo wa kushoto wa
mama yake baada ya kumlaza
mama yao
sakafuni kisha wakaukata
na panga
na kutokomea nao .
Hata hivyo baba
huyo mzazi amedai
mume aliyemuoa binti yake
huyo
aitwaye Gabriel
Yohana (43), kuwa ni
mwanaume katili kwa kumtuhumu
kumpiga mara kwa mara
mkewe huyo bila ya sababu za
msingi na
kumsababishia makovu mwili .Gabriel ana wake watatu
ambao wote kwa
pamoja wamemzalia
watoto 11 wote si albino.
Wakizungumzia mkasa huo
wake wenza wa Maria akiwemo
bi mkubwa aitwaye
Honoratha Xavier mama wa watoto sita
amedai kuwa usiku huo wa tukio
akiwa chumbani
na mume wao Gabriel ghafla aligutushwa na sauti kali
ambayo alidhani ni mlio wa fisi ambapo
alimwamsha mumewe ambaye
alichukua upinde na mshale
na kutoka nje .
“Ndipo baadaye tulipata taarifa kuwa mwenzetu
Maria ameumizwa na
majambazi walimvamia nyumbani kwake “ alisema .
Huku Esta Pesambili mama
ya mtoto mmoja ambaye ni mke wa pili
wa Gabriel
alidai kuwa yeye
binafsi hwakuwa na masikilizano na Maria kwa kuwa
ana wivu sana
ambapo alikumbuka katika mkasa mmoja wakati
wake wote
watatu wakishi katika nyumba moja katika kitongoji hicho
cha Mkoe
ambapo waligombana na Maria alijeruhi titi lake
la kulia kwa jembe .
“Ndipo kutokana
na kutoelewana kwetu Gabriel
aliamua kumjengea
nyumba yake peke yake Maria
na kumwamishia huko ndipo ukawa mwisho
wa ugomvi
wetu …. Licha ya kutoelewana
kwetu hakika nimesikitishwa
sana na
unyama aliofanyiwa na mwanamke mwenzetu” alisema kwa uchungu.
Kwa upande wake Zaina
kitindamimba wa mzee Chamanenge ambaye pia ni
albino amedai
licha ya kuwa na huzuni
kubwa kwa unyama aliofanyiwa
dada yake mbali ya
kuwa ni mwanamke lakini pia ni albino
mwenzake
lakini moyoni alifurahia kusafiri
hadi Sumbawanga mjini kumwona dada
yake huyo ambaye
bado amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa
akipatiwa matibabu.
“Sijawahi tangu
nizaliwe miaka 20 iliyopita kusafiri
umbali huu tena
kwa gari hii ni mara yangu ya kwanza ndio maana nimetapika njia nzima
sijawahi kusafiri
kwa gari
lakini baahati mbaya furaha yangu
hii
imegubikwa na majonzi
na huzuni kubwa moyoni “ alisema huku
akibubujikwa
na machozi.
0 comments:
Post a Comment