Alipokelewa kwa ngoma |
Alikutana na wadau kadhaa wa mauta mkoani Mtwara |
Hapo alipokuwa akienda ofisi kwa mkuu wa wilaya na pembeni ndio mkuu wa wilaya |
Mbunge wa Mtwara mjini Hasein Murji akimshukuru Millen kwa msaada wake ambapo na yeye alitoa mifuko 100 ya cement |
Hapa akiwa darasani mwanamitindi Millen alijiionea darasa hilo |
Hapoo ndo alikabidhi msaada wake kwa shule hiyo |
Nikiripoti kutoka hapa Mtwara ni mimi mdau wa elimu Evance wa Elimuboratanzania blog. |
Kutoka Mtwara:
MWANAMITINDO
mahiri wa kimataifa ambae pia aliwahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2001 Millen
Magese juzi alitoa milioni 15 kusaidia elimu kwa shule ya msingi ya Mjimwema na
Lilungu za mkoani Mtwara.
Millen alikabidhi
msaada huo kwa wa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Willman Ndile huku akishuhudiwa na
Mbunge wa Mtwara mjini Hasein Murji pamoja na wadau wengine wa maendeleo mkoani
humo.
Millen
akikabidhi hundi ya milioni hizo 15 baada ya kutembelea shule hizo na kujionea
hali hali ilivyo alisema kuwa msaada huo ni kutimiza ahadi yake aliyoiweka siku
moja angeenda mkoani humo na kusadia masuala ya elimu.
Awali
akitembelea shule ya Mji Mwema iliyopo kata ya Magengeni aliikuta shule hiyo
ikiwa katika hali duni ambapo kuna vyumba viwili vya udongo vya madarasa huku
kukiwa na wanafunzi wengi zaidi.
Millen
aliwaambia wazazi pamoja na wanafunzi waliokuwa katika shule hiyo kuwa ameguswa
na namna ambavyo hali ni mbaya katika eneo hilo na kuongeza kuwa yupo tayari
kuwa mlezi wa shule hiyo.
Alisema kuwa
ili wanafunzi waweze kusoma na kufikia malengo yao wanatakiwa kusoma katika
mazingira bora na yenye kuvutia ambapo alisema kuwa ni jukumu lake kuonesha
mfano katika hilo.
Aliwasihi
wazazi pamoja na wakazi wa eneo hilo kuhakikisha kuwa wasaidia katika ujenzi wa
shule hiyo kwa kujitolea kwa hali na mali kufanikisha ujenzi huo.
“ Iwapo
mkisaidi kuleta mchanga wengine wakafyatua matofali basi kila kitu kitaenda
sawa na tunaweza kujenga madarasa bora zaidi” alisema Millen.
Alisema kuwa
kwa sasa ameamua kuanzisha Taasisi yake iitwayo Happiness Millen Magese
Foundation kusaidia masuala mbalimbali
kama vile elimu, jinsia na harakati za maendeleo ya akimama.
Naye Mbunge
wa Mtwara mjini Hasein Murji alihamasika
zaidi na kuahidi kutoa mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya kufanikisha ujenzi
zaidi wa shule hiyo.
Alisema kuwa
kwa muda mrefu alikuwa akiumiza kichwa kutafuta namna ya kusaidia kujenga shule
hiyo na kwa msaada huo wa Millen ni hatua kubwa kwa maendeleo ya shule hiyo ya
Mjimwema.
Nae Mkuu wa
Wilaya ya Mtwara Willman Ndile aliwataka wananchi kuhamasika zaidi kwa kuunga
mkono harakati za Millen katika kuimarisha elimu mkoani humo kwa kuwa ameonesha
mfano mzuri akiwa kama mwanamitindo.
Pia millen
alimkabidhi mkuu huyo wa wilaya milioni tano kwa ajili ya ununuzi wa madawati
ya shule ya msingi Lilungu iliyopo kata ya Ufukoni Mtwara mjini.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment