Wanafunzi wa Mkwawa wakifurahia |
Wanafunzi wa Uganda wakihamasishana |
Wadau kutoka Zantel wakifuatilia mashindano hayo |
Waziri wa vijana, utamaduni na
michezo, Fenella Mukangara akisalimiana na Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid
Khan wakati wa uzinduzi wa michezo ya vyuo vikuu Afrika Mashariki. Katikati ni
Meneja Mkuu wa mawasiliano wa Zantel, Awaichi Mawalla.Zantel ni mojawapo wa
wadhamini wa michuano hiyo.
Habari Kamili
WANAFUNZI wa
vyuo vikuu vya Afrika Mashariki wametakiwa kuwa vinara katika kuhamasisha amani
na usalama kwa njia ya michezo katika nchi zao.
Wito huo
ulitolewa jana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fennela
Mukangara wakati akifungua michuano ya siku tano michezo mbalimbali ya vyuo
vikuu vilivyopo katika nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki iliyoanza jana katika
viwanja vya Chuo Kikuu Dar es salaam..
Fennela aliwataka wanafunzi hao wanaoshiri michezo
hiyo kuhakikisha kuwa mbali na kushiriki michezo hiyo pia wanawajibu wa
kuhakikisha kuwa wanajadili masuala mbalimbali ya amani na namna ya kuidumisha.
Pia Fenella
aliwataka wanafunzi hao kuwa mabalozi wazuri katika kudumisha jumuiya ya Afrika
Mashariki kwa kujadiliana namna mbalimbali ya kudumisha ushirikiano huo.
Alisema kuwa
wanaweza kubadirishana mawazo ya namna ya kuboresha mazingira katika sekta
mbalimbali ya jumuiya ya Afrika Mashariki na aliwataka kuhakikisha kuwa
wanakuwa mfano bora kama vijana katika kufanikisha hilo.
“ Mkiwa kama
vijana mnalo jukumu kubwa kuhakikisha kuwa mnatumia michezo hii katika
kudumisha amani na upendo katika jumuiya kwa kuwa kama mnavyofahamu kuwa
michezo ndio moja kati ya njia za kipekee zinazowaweka pamoja wanajamii na
hivyo nyie mkiwa kama vijana huu ni wakati wenu kujadilia masuala ya amani pia”
alisema Fennela.
Kwa upande wake Ofisa Biashara Mkuu wa kampuni ya mkononi ya
Zantel inayodhamini michuano hiyo Sajid Khan alisema kuwa kampuni hiyo inatambua
umuhimu wa michezo katika vyuo vikuu kwa kuwa wanafunzi hao ndio wanakuja kuwa
wafanyakazi wa baadae hivyo wakijiandaa kimichezo wkaiwa vyuoni inaongeza afya
na utendaji unakuja kuwa mzuri wakianza kazi.
Naye Naibu
Makamu Mkuu wa Chuo Yunus Mgaya alisema kuwa michezo hiyo iliyoanza jana itaendelea
hadi februali 12 katika viwanja vya chuo hicho.
Alisema kuwa
michuano hiyo inahusisha michezo mbalimbali kama vile riadha, kuogolea, mpira
wa miguu, pete, kikapu netiboli na michezo mingine.
Alisema kuwa
kwa hapa Tanzania vyuo vilivyoaliwa ni saba huku Uganda vikiwa vyuo 17 na Kenya
vyuo 17 pia lakini hata hivyo gaezti hili lilishuhudia vyuo vya kutoka hapa
nchini ni Chuo Kikuu Huria na Chuo Kikukuu cha Mkwawa peke yake vikiwa
vimewasili katika viwanja hivyo.
0 comments:
Post a Comment