hatimaye imeonesha usikivu kwa kukubali maoni ya wadau mbalimbali wa elimu
nchini na kuunda Tume Maalumu itakayochunguza matokeo ya mtihani wa Kidato cha
Nne.
Matokeo hayo
yaliyotangazwa Februari 18 na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru
Kawambwa, yalionesha watahiniwa asilimia 60 kufeli mtihani huo uliofanywa Oktoba
mwaka jana, na kuzua maswali kwa wadau.
Baada
ya wadau hao wakiwamo viongozi wa vyama vya siasa na Serikali kupendekeza
kuchukuliwa hatua kuhusiana na matokeo hayo mabaya kupata kutokea katika
historia ya elimu nchini, Serikali imeridhia na kuitikia mwito huo.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lyimo katika taarifa yake jana, alisema Tume
hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kazi wakati wowote wiki ijayo, inajumuisha wadau
kutoka Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi (TAMONGSCO), taasisi za dini
zinazotoa huduma ya elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Asasi Zisizo za
Serikali (AZISE) zinazoshughulikia elimu.
Wadau
wengine watatoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Kamati ya Bunge ya Huduma za
Jamii na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA).
Aliwaomba
wadau wa elimu, wazazi, walezi na wananchi kwa ujumla wao watoe ushirikiano kwa
Tume ili iweze kufanya kazi yake kwa ufanisi.
Hata
hivyo, Lyimo katika taarifa yake fupi, hakutaja majina ya watakaounda Tume hiyo
wala muda itakayopewa kukamilisha kazi yake.
Matokeo
Akitangaza
matokeo, Dk Kawambwa alisema zaidi ya nusu ya
wanafunzi waliofanya mtihani
wa
Taifa wa Kidato cha Nne, wamepata daraja sifuri na kufafanua, kwamba kati ya
wanafunzi
397,
136 waliofanya mtihani huo, 240,903, ndio waliopata daraja sifuri.
Alisema
waliopata daraja la kwanza ni 1,641, la pili 6,453 na la tatu 15,426 na
kuongeza kuwa wanafunzi 24 ambao matokeo yao
yalifutwa kwa kuandika matusi kwenye masomo
mbalimbali wakionesha utovu wa nidhamu wa hali
ya juu na kwamba Serikali haitavumilia.
“Tunaangalia hatua za kisheria za
kuchukua dhidi yao. Na kwa wale
waliofanya udanganyifu wanaweza
“Ukiangalia zilizofanya vibaya,
ni zenye changamoto ya kukosa walimu hususan wa Sayansi
na Hisabati, kutokuwapo kwa
maabara za shule na upungufu mkubwa wa vitabu vya kiada na ziada na kuwa na
uwiano wa kitabu kimoja kwa wanafunzi 10,” alisema.
Iundwe Tume
Baada ya
kutangaza matokeo hayo, chama cha NCCR-Mageuzi kupitia Mwenyekiti wake, James
Mbatia, kilimwomba Rais Jakaya Kikwete aunde Tume itakayojumuisha wataalamu
waliobobea katika elimu ili kupata suluhu ya kuendelea kushuka kwa elimu, kwa
kuwa limekuwa janga la kitaifa.
Kwa upande
wake, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa naye alipendekeza iundwe Tume
kuchunguza hali hiyo ya idadi kubwa ya wanafunzi kufeli mtihani huo.
“Matokeo ya Kidato cha Nne yamenisikitisha
sana maana asilimia 60 ya wanafunzi kupata sifuri ni jambo la hatari. Napenda
kumsihi Rais Kikwete, amefanikiwa katika sekta nyingine kama barabara… aunde
tume kuchunguza sababu za wanafunzi kufeli, lakini kubwa kuliko zote tume hiyo
ije na mapendekezo ya namna bora ya kuboresha mfumo wetu wa elimu,” alisema Lowassa.
Alisisitiza kuwa hoja ya kutaka Serikali
iunde tume kuboresha mfumo wa elimu, alipata kuitoa mara kadhaa kwani anaamini
katika kaulimbiu ya ‘Elimu Kabla, Kilimo Kwanza’.
“Kila Mtanzania anasema lake, wengine
wanasema ni hujuma, wengine wanadai kuna mgomo baridi wa elimu, malalamiko na
sababu ni nyingi na njia pekee ya kujua ukweli ni kupitia tume,” alipendekeza
Lowassa.
Kurudia
mtihani
Wakati hayo
yakiendelea, Serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Philipo Mulugo imesema inaangalia utaratibu wa watahiniwa waliopata daraja
sifuri kurudia mtihani mwaka huu kwa gharama zake.
Aidha, ikasema matokeo hayo
mabaya yamesababishwa na mambo makuu manane; kubwa likiwa ni wanafunzi kupita
bila kuchujwa katika mtihani wa Kidato cha Pili walioufanya miaka miwili
iliyopita.
Ingawa hata hadidu za rejea kwa
tume hiyo hazikutajwa jana, pengine zikisubiri izinduliwe rasmi, ni dhahiri
pamoja na mambo mengine, itachunguza pia chanzo cha watahiniwa badala ya kujibu
maswali, wamekuwa wakiandika matusi na kuchora vibonzo.
Pia itaweza kuchunguza utendaji
kazi wa walimu na kuhusiana na migomo, lakini hasa kutafuta suluhu ya nini
kifanyike kuhakikisha wanafundisha katika mazingira mazuri, huku wanafunzi nao
wakijibidiisha katika masomo yao.
Suala la uwiano wa walimu na
wanafunzi, pamoja na vifaa vya kufundishia na kujifunzia na maabara, huenda
nalo likawamo hususan katika shule za sekondari ambazo nazo zimezua mvutano
miongoni mwa wadau kuhusu hoja ya kujengwa bila maandalizi ya kutosha.
mwisho