Meneja wa Habari, Mawasiliano na Elimu wa TEA Sylvia Lupembe akimkaribisha mgeni rasmi Waziri Shukuru Kawambwa
Baadhi ya wajumbe wa bodi mpya ya TEA wakipongeza hotuba ya Waziri
Picha ya pamoja kati ya Waziri Kawambwa na wajumbe wa bodi ya TEA na Waziri Kawambwa
.
Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi Shukuru Kawambwa akimkabidhi makablasha ya kazi
Mwenyekiti wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Naomi Katunzi wakati wa uzinduzi
wa Bodi Mpya ya mamlaka hiyo katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa TEA Rose Rulabuka.
Waziri Kawambwa aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Bodi ya TEA jana alisema kuwa ili TEA kuendelea kufanya kazi zake kiukamilifu ni vema ikawa na vyanzo vyake vya mapato
Kawambwa alisema kuwa licha ya kazi nzuri ambayo bodi hiyo imeifanya katika kuongeza ubora wa elimu nchini ikiwa pamoja kuhakikisha upatikanaji wa kwa usawa ni vema ikatambua kuwa inalo jukumu la kuishauri serikali juu ya vyanzo vya uhakika vya mapato.
Pia aliipongeza mamlaka hiyo kwa kuratibu miradi 1,290 ya elimu ambayo imeratibiwa na kufanyiwa kazi kwa ufanisi wa hali ya juu ikiwa na thamani ya Shilingi bilioni 36.7 za kitanzania.
" Ninatambua kuwa TEA ina majukumu mengi kulingana na sheria Namba 8 ya Mfuko wa Elimu ya mwaka 2001 ambapo mnatakiwa kutafuta rasilimali kwa ajili ya Mfuko wa Elimu na Kuratibu matumizi ya rasilimali hizo kwa ajili ya kufadhiri miradi ya elimu nchini " alisema Kawambwa
Jana Waziri huyo alizindua bodi yenye wajumbe nane huku Naomi Katunzi akiendelea kuwa Mwenyekiti wa bodi hiyo kwa mara ya pili.
0 comments:
Post a Comment