Na Mwandishi Wetu
KWA muda mrefu sekta ya sanaa nchini
imekuwa ikichukuliwa kuwa ni sekta isiyokuwa na tija kubwa kwa maendeleo ya
nchi.
Sekta hii imekuwa ikionekana kuwa ni
kama vile sekta ambayo ina umuhimu wa kuburudisha tu kwa njia ya nyimbo katika
majukwaa na tena sio kufikia kwa kiwango cha kushiriki kikamilifu katika miradi
ya elimu kwa njia ya sanaa.
Kwa sasa dhana hiyo imeanza kufutika
kufuatia wasanii wanaoshiriki katika muziki wa kizazi kipya wameanza kushiriki
katika miradi mbalimbali ya elimu kwa jamii.
Miradi hiyo ni kama vile ya utoaji
elimu kwa njia ya Malaria unaotekelezwa na wasanii wa Tanzania House of Talent
(THT) ambao ni watekelezaji wakuu wa mradi wa Zinduka.
THT imeweza kuifikia jamii nyingi za
kitanzania na kuzielimisha kwa kuzingatia
mahitaji na mazingira waliyomo katika jamii inayowazunguka.
Kwa kutumia sanaa ya maigizo THT
imeweza kuwaelimisha kirahisi wanafunzi pamoja na walimu pia na hata wanajamii
na hivyo kuweza kudhihirisha kuwa muziki ni kiungo muhimu katika elimu.
Hayo yanajidhihirisha katika ziara
yao ambayo inaendelea katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ambapo wasanii hao kwa
pamoja wameweza kushirikiana na Mgodi wa Afrika Barick kuwalinda wananchi dhidi
ya ugonjwa wa Malaria.
Nguvu iliyopo katika sanaa ni kubwa
mno kwa kuwa licha ya kuwaelimisha wananchi lakini pia wananchi wanapata
burudani ambayo inawapa moyo wa kuendelea kusikiliza ujumbe lakini pia hata
kukumbuka kirahisi yale waliyofundishwa.
Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa la
Taifa (BASATA) Ghonche Materego aliwahi kusisitiza umuhimu wa ngoma za asili,
maigizo na hata nyimbo za kizazi kipya katika kuifikia jamii na kuielimisha.
Anafafanua kuwa muziki unaweza kuwa
na ujumbe zaidi ya mmoja kwa kuwa wanamuziki wanaweza kufikisha ujumbe kwa
kutumia miili yao na hata kwa kutumia sauti na njia nyingine muhimu.
Wasanii wa THT wameweza kuifikia
mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera na Shinyanga ambapo wasanii hao wa THT
wametembelea sekondari katika mikoa hiyo na kuimarisha klabu za Malaria kwa
wanafunzi.
Martini Genos ni mratibu wa elimu ya
Malari aya THT shuleni anasema kuwa kwa sasa wamemaliza ziara yao katika Mkoa
wa Kagera na wameshaingia Shinyanga ambapo walianzia mkoa wa Mara na baadae
wakafuata Mwanza.
Anasema kuwa kupitia muziki wameweza
kuhamasisha wanafunzi pamoja na watu wengine katika jamii na kuwafundisha
masuala mbalimbali kupitia ngoma, nyimbo za asili na za kisasa pamoja na
maigizo.
Anasema kuwa nguvu iliyopo katika
sanaa za maigizo na nyimbo ni kubwa kwa kuwa imewaweka karibu na wanajamii na
wanafunzi wa mikoa hiyo kiukaribu zaidi na kuwapatia elimu.
Anatolea mfano kuwa katika mkoa wa
Mara waliwafikia wanafunzi 7500 huku wanajamii wanaohudhuria matamasha yao nao
pia wakiwa 2000 ambapo wasanii nane kutoka THT walishiriki kikamilifu katika
kutumia vipaji vyao kubadilisha mitazamo potofu ya wannachi kuhusiana na asili
ya ugonjwa wa Malaria kuanzia maambukizi yake mpaka namna ya kuutibu.
“ Kwa kawaida tunawauliza wanaliza
wanafunzi maswali mbalimbali kwa lengo la kupima uelewa wao katika masuala ya
Malaria na kuanzia hapo ndio tinaona ni njia gani ya kuanza kuwaelimisha juu ya
ugonjwa huu” anasema Martin.
Anasema kuwa wanatumia siku chache
wanapokuwa katika jamii za mikoa hiyo kuwauliza wanafunzi kuhusiana na uelewa
wao wa ugonjwa wa Malaria a kubaini kikwazo kikubwa cha ugonjwa huo na kisha
kutunga igizo.
Licha ya wasanii hao kuwa na maigizo
yao kuhusiana na namna ya kupambana na Malaria lakini pia wanaweza kutunga upya
au kuongezea vionjo mbalimbali vinavyowaweka wanafunzi kuwa karibu zaidi na
igizo hilo.
Martini anasema kuwa katika maigizo
hayo wasanii wa THT wanaweza hata kuingiza maneno ya kilugha katika mikoa
wanapokuwa wanatoa elimu ya Malaria ilimradi kuwaweka karibu walengwa ambao ni
wanafunzi wa Sekondari katika mikoa hiyo.
Akizungumzia Sekondari ambazo
wasanii wa THT wametoa elimu kwa njia ya sanaa mkoani humo anasema kuwa
waliwasili katika Sekondari ya Lubondo iliyopo wilayani Biharamulo, Sekondari
ya Chato iliyopo Chato, Sekondari ya Bukoba iliyopo Bukoba mjini na sekondari ya Kishoju iliyopo Muleba.
Akizungumzia namna ambavyo THT
inaweza kubadilisha mawazo kama hayo anasema kuwa wasanii hao wanaweza kutunga
maigizo ya kukemea hali hiyo huku wakitumia mifano hai katika jamii kama hiyo.
Anasema kuwa ili kupambana na imani
kama hizo THT licha ya kutoa elimu ya malaria lakini pia inaandaa klabu za
malaria kwa wanafunzi katika kila shule ambayo imetembelea.
Akizungumzia hamasa ya wanafunzi
katika kuvutiwa na sanaa za THT katika kupata elimu anasema kuwa THT mkoani
Kagera wanafunzi wamekuwa hawana tofauti sana na mikoa mingine waliyokwisha
kwenda kwa kuwa kwanza walionekana kuvutiwa sana na sanaa iliyotumika pia.
Pia alisema kuwa uelewa kwa
wanafunzi kuhusiana na malaria ni mkubwa isipokuwa kuna masuala muhimu ambayo
yalikuwa ya kuongezea katiak suala la elimu kwa wanafunzi.
kazi ya uelimishaji ilianzia Mara
katika Sekondari ya Dk Nchimbi iliyopo
wilaya ya Bunda na ndipo walipoanza kujipanga na kujua ni nini zaidi wanatakiwa
kuwapatia wananchi.Kundi hilo la THT pia lilielimisha na kuburudisha Sekondari
za Buhita ya Musoma vijijini, Nkende ya Tarime Malenge ya Musoma vijijini na
Nyandega iliyopo wilaya ya Rolya.
0 comments:
Post a Comment