Mratibu wa promosheni ya tigo katikaElimu Edward Shila akikabidhi msaada wa Kompyuta kwa Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Profesa Shaaban Mlacha juzi. Jumla ya Kopyuta 48 zenye thamani ya zaidi ya Sh 37 Milioni zilikabidhiwa na kampuni hiyo kwa ajili ya Kitivo cha sayansi ya tiba kwa jamii. (Picha na Kwa hisani ya Tigo)
Na Mwandishi wa elimu bora kutoka Dodoma.
Tigo imetoa
msaada wa kompyuta 48 kwa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) kama sehemu ya kuboresha
sekta ya elimu na kusaidia matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano
(Tecknohama).
Hafla ya
makabidhiano hayo imefanyiaka leo katika chuo kikuu cha Dodoma. Kompyuta
zilikabidhiwa kwa niaba ya Tigo na mratibu wa Promosheni na Matukio Bwana
Edward Shila. Akizipokea kwa niaba ya chuo,kaimu makamu
mkuu mipango, fedha na utawala, Prof. S.A.K.Mlacha ameshukuru Tigo kwa msaada
huo na kusema kuwa kompyuta hizo zitasaidia kuboresha mahitaji ya Tecknohama
chuoni hapo.
“Ili tuweze
kukabiliana na ushindani duniani,wanafunzi wanahitaji kuwa na uelewa juu ya
kompyuta na tecknohama,” alisema Prof. Mlacha. “Msaada huu utawaunganisha na
taarifa na tecknolojia kama njia ya kusoma na kupata taarifa ya yale
yanayoendelea katika masomo yao,” alisema.
Bw. Shila
alisema, “Teknolojia imekuwa ni sehemu kubwa ya maisha yetu, elimu na kazi.
Tigo imefurahia kutoa komputa na vifaa vingine kwa viongozi wetu wajao.”
0 comments:
Post a Comment