TAASISI ya
kifedha ya Bayport hapa nchini, imeendelea kutoa msaada wa vitabu kwa shule ya
Sekondari Mpindimbi ili viwasaidie kukuza kiwango cha elimu nchini.
Makabidhiano hayo
yalifanyika katika viwanja vya shule hiyo na kupokelewa na Ofisa Elimu wa
Wilaya ya Masasi kwa shule za sekondari, Generosa Nyoni.
Akizungumza
katika makabidhiano hayo mjini hapa jana, Meneja wa Kanda ya Kusisni, Aidan
Kessy, alisema msaada huo ni endelevu kwa shule 20 na kwa wilaya zisizopungua
20 kwa mikoa ya Tanzania Bara.
Alisema wanaamini
kwa kutoa msaada huo wa vitabu kwa shule hiyo ya Mpindimbi, walimu na wanafunzi
wataweza kuvitumia vizuri kwa ajili ya maendeleo ya elimu nchini.
“Huu ni mkakati
endelevu uliobuniwa maalum kwa ajili ya kuwapatia wanafuunzi urahisi kwenye
shughuli zao.
“Naamini mambo
utakuwa ni mpango mzuri na wenye tija kwa kuhakikisha wanafunzi wanapata dhana
za kujifundishia ili waelimike zaidi,” alisema.
Naye Ofisa Elimu
wa Wilaya kwa shule za sekondari mjini Masasi, Generosa Nyoni, akiwashukuru
Bayport kwa kuwasaidia vitabu kwenye eneo lao.
“Tunashukuru na
wengine waige mwendo huu maana ndio utakaowawezesha wanafunzi wamudu masomo
vizuri, “ alisema.
Tayari shule
mbalimbali zimenufaika kwa mpango huo wa kutoa msaada wa vitabu ulioanzishwa
mwaka jana.
0 comments:
Post a Comment