Zaidi ya watu
wapatao mia moja walishiriki katika matembezi ya kujitolea katika ufunguzi wa
kampeni ya Tigo Tuchange kwa ajili ya kukusanya hela ya kuchangia sekta ya
elimu nchini Tanzania.
Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya ufundi, Mh. Shukuru Kawambwa alizindua matembezi hayo Machi 3, 2012,
kwa kukata utepe na kuwaongoza watembeaji kutoka Shekilango
Millenium Bussiness Complex hadi Ubungo mataa. Nchini kote, maelfu ya watu
walijitokeza na kuongeza muda wa maongezi kupitia Tigo Rusha ili kuchangia
kampeni hii.
“
Ningependa kuwashukuru wote walioshiriki kuchangia kampeni ya mwaka huu”
alisema Bw. Diego Gutierrez, ambaye ni Meneja Mkuu Msaidizi wa kampuni ya Tigo.
“ Tunafuraha kufahamu kuwa matokeo ya juhudi zetu za pamoja zitaleta mabadiliko
kwamamia ya watoto wa shule nchini” alisema.
Shiling
milioni 26 zimekusanywa kupitia muda wa maongezo ulionunuliwa kupitia
Tigo Rusha Kati ya saa tano na saa sita mchana wa siku hiyo.
Wateja
walionunua muda wa maongezi kati ya muda huo, waliweza kutumia muda wao wa
maongezi kama kawaida wakati Tigo ilirudufu kiasi hicho na kuingiza
katika kampeni hiyo ya uboreshaji wa Elimu.
Fedha zote zilizopatikana katika
tukio hilo zitapelekwa kwa Hassan Majaar Trust (HTM), programu endelevu yenye
lengo la kuboresha mazingira ya upatikanaji wa elimu kwa kutoa
madawati kwa shule mbalimbali zenye uhitaji.
Mwenyekiti
wa HTM, Balozi Mwanaidi Maajar, alisema “Tumefarijika sana na kampeni hii na
tungependa kuwashukuru Tigo kwa mchango huu utakaosaidia mahitaji ya elimu kwa
watoto wa Tanzania.
Msaada huu tulioupata leo utatumika katika kununulia
madawati kwa shule mbalimbali ambazo tunazo na tumethibitisha kuwa na uhitaji.
Lengo letu ni kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anakaa kwenye dawati. Tunaona
kwamba hii ni hatua kubwa katika kufikia malengo yetu”.
0 comments:
Post a Comment