"Ili muweze kuwa wanamitindo bora ndani na nje ya nchi inatakiwa kwanza mjiamini, mnasikia? na pia kuzingatia yale niliyowafundisha"
Mkiwa mbele ya watazamaji katika shoo mnapomaliza kutembea mnatakiwa kupozi hivi sawa?
Sikia mdogo wangu huwa hizi nyusi zinatengenezwa hivi sawa?
Na Mwandishi wa Elimu Bora Tanzania.
Mkiwa mbele ya watazamaji katika shoo mnapomaliza kutembea mnatakiwa kupozi hivi sawa?
Sikia mdogo wangu huwa hizi nyusi zinatengenezwa hivi sawa?
Na Mwandishi wa Elimu Bora Tanzania.
WABUNIFU watatu wa mavazi nchini watawakilisha
Tanzania katika maonesho makubwa ya mavazi ya Afrika Kusini yatakayoshirikisha
wabunifu kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Wabunifu hao wamechaguliwa kutoka katika mpango wa
kuendeleza wanamitindo na wabunifu wa mavazi ulioanzishwa na mwanamitindo
mtanzania anayefanya shughuli zake nchini Afrika Kusini Millen Magese kupitia
kampuni yake ya Millen Magese Group company Limited.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Millen alisema
kuwa mpango huo umeanza kuwa wa mafanikio kwa kuwa ameweza kuwapata wabunifu
wazuri pamoja na wanamitindo wenye mvuto.
Aliwataja wabunifu hao kuwa ni Doreen Noni anayetumia Lebo
ya eskado bird, Jamila Vera Swai na Evelyne Rugemalira ambao watapanda
jukwaani April Mosi ambapo watawakilisha katika kipengele cha Tanzania
International Fashion Exposé (TIFEX).
Alisema kuwa kabla ya kuwachagua alipata fursa ya
kutembelea wabunifu hao na kujionea jinsi walivyokuwa wabunifu katika fani hiyo
na kuhamasika kuwachukua na kushiriki katika maonyesho hayo maarufu ya mitindo
katika bara la Afrika.
Alisema kuwa amevutiwa sana na jinsi walivyokuwa
wabunifu na hivyo kuhamasika kuwapa nafasi hiyo ya kujitangaza kimataifa kwa
mara ya kwanza katika historia ya Tanzania kupitia mradi huu anbao pia dhumuni
lake kutangaza vivutio vya utalii wa Tanzania kimataifa.
Alifafanua kuwa mpango huu pia una lengo la kuitangaza
Tanzania kupitia fani ya mitindo dunia nzima kama New York fashion week, London
Fashion Week, Lagos Fashion week na Milan Fashion week.
Kwa upande wa wanamitindo waliochaguliwa ni Anastazia Gura (21) huku wengine waeili wakiwa
ni mapacha,Victoria Casmir (20) na
Victor Casmir ambao wao walichaguliwa kutoka katika zoezi la kuwachagua
wanamitindo lililofanyika Jumapili iliyopita.
Katika kuonesha nia ya kweli ya kusaidia mitindo hapa
nchini Millen pia ameingia mkataba wa kufanya kazi na mwanamitindo wa kiume,
Benard Chizi ambaye atakuwa akisaidiana naye katika kazi zake.
Mwisho.