Akitambulishwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Michezo bwana Dennis kwa waandishi wa habari |
Hapa kazi ilianza ya kucheza |
Akionesha manjonjo yake |
Picha ya pamoja na wadau wa mchezo huo |
Mkurgenzi wa Maendeleo ya Michezo akizungumza na Mama anaemlea Kondo huko Marekani |
Mimi (kushoto) Kondo na mwandishi wa Nipashe |
Akiwa na mdhamini wake |
Wdsau wakipiga nae picha huyo mama wa kizungu ndo alimlea |
Timu aliyoenda nayo huko Maekani lakini hawa walitokea hapa hapa bongo |
Anaruka balaa |
Na Evance
Ngingo
KIJANA
Khamis Kondo (14) ameshinda michuano ya dunia ya kuruka kamba iliyofanyika
nchini Marekani Julai 5 hadi 13 nchini Marekani.
Shindano
hilo lilishirikisha nchi 14 pamoja na timu 44 ambapo wachezaji walikuwa 480.
Akizungumza
katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jana Kondo alisema kuwa alikuwa
akitumia saa tano kujifua katika kituo cha Seattle Jump kilichopo Seattle
nchini Marekani.
Alisema kuwa
akiwa kwenye mashindano hayo alitumia mbinu mbalimbali za kucheza mchzo huo
hali iliyopelekea ushindi wake.
"
Kutokana na kujifua kwa miezi sita kwenye kituo hicho nilipata ujuzi wa kujua
namna ya kucheza mchezo huo wa aina yake na ndio nikajikuta ninaliletea taifa
langu ushindi mkubwa kama huu" alisema Kondo.
Alisema kuwa
kila siku baada ya kutoka shule ya Amy Canady anayosoma nchini humo alikuwa
akirudia kwenye kituo hicho na kujifua chini ya uangalizi wa mwalimu wake.
Kondo
alishiriki na washiriki wengine waliotokea moja kwa moja katika kituo cha
dogodogo Center ambao ni Joshua John, Emanuel Joseph, Athuman Sungi na Furaha
Mwakisyala.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo Cha Michezo Tanzania, Dennis Makoi ambae kituo chake
kilishirikiana na Dogodogo Center alipikuwa akilelewa Kondo alisema kuwa
ushindi wa Kondo umepelekea kituo chake kupatiw amisaada ya kimichezo.
Alisema kuwa
kituo hicho baada ya kumuona kijana huyo akishinda kwenye mashindano ya kuruka
kamba ya nchini Kenya mwaka 2010 kiliamua kumuombea udhamini nchini Marekani
kwenye kituo cha mafunzo cha Seattle Jump.
Alisema kuwa
ushindi alioshinda ni katika michuano iliyofanyika Julai 5 hadi 13 mwaka huu na
kushirikisha washiriki kutoka nchi 14 huku kukiwa na timu 44 na wachezaji zaidi
ya 300.
"Hii ni
hatua nzuri na ya kimafanikio kwa kuwa hata hapo kituoni nchini Marekani
anapojifunza amewashinda hata wanafunzi wenzake waliojitokeza kushiriki mchezo
huo wa aina yake sasa hiki ni kipaji ambacho tunatakiwa ujivunia na
kukiendeleza." alisema Makoi.
Pia
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Idara ya Michezo iliyopo kwenye Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo nchini Juliana Yasoda alitoa wito kwa
wadau wa michezo kuwekeza kwenye mchezo huo.
Yasoda
alisema kuwa michezo ambayo sio maarufu kama huo wa kuruka kamba ni moja kati
ya michezo ambayo inaweza kuwekezwa na kulisaidia taifa kufikia katika ngazi ya
kimataifa.
Alisema kuwa
kwa hatua ya mshindi wa dunia wa mwaka huu wa mchezo wa kuruka kamba kushinda
huku akiwa na miaka 14 ni inashara nzuri kuwa mchezo huo unaweza kulitangaza
taifa.
" Sasa
kama huyu akiwa na miaka 14 na amejifunza kwa miezi sita tu nchini Marekani
kucheza mchezo huu basi inamaana kuwa anaweza kufika mbali hasa mwakani kwenye
Olimpiki ambapo mchezo huu utakuwapo" alisema Yasoda.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment