WANAFUNZI wa kike wanaosoma katika Shule ya Sekondari Mzindakaya
kijijini Kaengesa wilayani Sumbawanga mkoani hapa wamekiri kufanyiwa
visa vya udhalilishaji mara kwa mara muda mrefu sasa lakini wamekuwa
wakiona aibu kuripoti visa vya ubakaji wanavyofanyiwa kwa uongozi wa
shule pia kwa wazazi wao .
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni umebaini
kuwa wanafunzi hao wa kike ambao wanapanga vyumba katika nyumba
ambazo ni mbovu wamekuwa wakibakwa mara kwa mara na watu ambao wao
wenyewe wanadai ni vijana maarufu kama ‘wezi wa mafuta ‘ waliozagaa
kijijini humo kutoka maeneo mbalimbali mkoan humo wakishirikina
na baadhi
ya wakazi wa kijiji hicho .
Vijana hao ambao wanadaiwa kujihusisha na wizi wa mafuta ya
kuendeshea magari na mitambo kutoka katika Kampuni ya Ujenzi wa barabara
ya kutoka mjini mdogo wa Laela mpaka Sumbawanga mjini kwa kiwango cha
lami .
Uchunguzi huo umebaini kuwa wengi wa wanafunzi hao wa kike
wamelazimika kupanga vyumba kwa bei ya kutupa ya sh 1,000- kwa mwezi
kutokana na wazazi wao kukataa kuchangia gharama ili watoto wao hao
waweze kuishi katika mabweni mawili yaliyopo shuleni hapo ambapo sasa
yamelazimika kubakia tu wazazi hao wakidai kuwa ni maskini .
Baadhi ya wanafunzi hao wa kike waliohojiwa na mwandishi wa habari
hizi hivi karibuni shuleni hapo walikiri kukumbwa mara kwa mara na visa
vya kubakwa lakini wanaogopa pia kuona aibu kutoa taarifa kwa mamalaka
husika hivyo wamebakia kukaa kimya na kujiuguza kisirisiri .
“Wengi wetu hatujui hatima yetu kwani tunaishi kwa hofu kubwa hususani
ifikapo usiku tunakosa raha licha ya kwamba kila mmoja wetu
amepanga chumba lakini kutokana na visa vya kubwaka mara kwa mara
tumeamua kulala chumba kimoja wasichana kati ya watatu hadi sita .
Tatizo ni wazazi wetu hawataki tuishi katika mabweni shuleni eti wao
ni maskini hawawezi kuchangia gharama za sisi kuishi bwenini ..... tuna
hofu kubwa basi tu kwani tunabakwa lakini hatuwezi kusema tunaona aibu
......” alisema mmoja wao.
Mwandishi wa habari hizi hivi karibuni alitembelea baadhi ya nyumba
walizopanga watoto hao wa kike na kushuhudia zikiwa katika hali mbaya
zingine zikiwa hazifai kuishi binadamu kwani hazina vyoo wala sehemu
ya kupikia chakula pia hazijazungushiwa kuta kwa ajili ya usalama
wa wapangaji
wa nyumba hizo .
“Kama unavyoona nyumba choo kilichopo ni kibovu hakina hata mlango
na kiko nje mita kadhaa kutoka katika nyumba hii hivyo kutokana na
hofu ya kutoka nje kuijisaidia wakati wa usiku tunalazimika
kujisaidia kwenye makopo tunayoyahifadhi vyumbani kisha asubuhi
tunaenda kumwaga uchafu huo chooni .....” alibainisha mmoja wao.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi shule ni hapo hivi karibu
Makamu Mkuu wa shule hiyo , Agatha Okumu alikiri kuongea na wanafunzi
wa kike wanaosoma shuleni hapo ambao wanaishi katika nyumba za
kupanga kijijini hapo kuwa kumekuwepo na visa vingi tu vya kubakwa
kwa wanafunzi hao lakini wamekiri kuwa wamekuwa wakifisha kusema
kwa kile
wanachodai kuwa wanaona aibu kusema .
“Nyumba walizopanga hazifai wao kuishi kwani hazina usalama
kwani kutokana
na milango ya vyumba wanavyoishi kuwa mibovu usiku wanafunzi hao
wanalazimika kuegesha vinu kuzuia isifunguke lakini imekuwa ni rahisi
sana kwa ‘wabakaji ‘ kusukuma tu milango hiyo na kuingia ndani kisha
kuwaingilia na kutokomea kusikojulikana “ alibainisha .
Aliongeza kuwa visa vya kubakwa wanafunzi hao wa kike ni vingi
lakini ni vitatu tu vilivyoripotiwa hadi sasa ambapo kisa cha kwanza
kiliripotiwa baada ya wanafunzi watatu kubwakwa na mtuhumiwa alisakwa
na kumatwa na kufikishwa katika vyombo vya dola .
Kwa mujibu wa Makamu huyo wa Mkuu wa Shule hiyo , Okumu alitaja visa
vingine ni pamoja na mwanafunzi wa kidato cha nne shuleni hapo
alijiua kwa kunywa sumju ya panya baada ya kubakwa na mwenzake na
mtu asiyefahamika baada ya mtu huyo kuwavamia chumbani mwao walimokuwa
wakiishi watatu nakuwatishia kuwaua iwapo wangepiga kelele .
“Haya juzi tu wanafunzi sita waliokuwa wakiishi chumba kimoja
wamenusurika kubakwa na watu wawili waliowavamia usiku wakiwa
wamelala chumbani mwao ........ lakini walishindwa kuwafanyia vitendo vya
udhalilishaji baada ya kuwakuta kuwa ni wengi na walianza kupiga mayowe
ndipo walipowapora kiasi cha Sh 1,100- walizokuwa nazo kisha wakawapiga
kwa marungu na kutokomea kusikojulikana “ alibainisha .
Hata hiyo baadhi ya wanafunzi hao na Mkuu wa Shule hiyo Nicholas
Thomas wamewatupia lawama wakazi hususani majirani wanaoishi karibu
na nyumba
walizopanga wanafunzi hao kwa kutowapatia msaada wowote licha
ya waokupiga
mayowe ya kuomba msaada .
“Kukicha ndipo wanapokuja na kutupa pole huku wakidai kuwa licha ya
kutusikia tukipiga mayowe ya kuomba msaada wanashindwa kutoka nje kwa
hofu ya kushambuliwa na watu hao wasiojulikana “ alisema mmoja wa
wanafunzi hao kwa masikitiko .
Kwa mujibu wa Mkuu wa Shule , Thomas wazazi wanatakiwa kuchangia gharama
za watoto wao kuishi katika mabweni shuleni hapo ambapo kwa mtoto mmoja
kwa muhula mzazi anatakiwa kuchangia magunia mawili ya mahindi, debe
moja la maharagwe na Sh 40,000- ikiwa ni ujira wa mpishi .
Mwisho
0 comments:
Post a Comment