MSANII wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnum amemaliza ziara yake ya kikazi na kimasomo nchini Afrika Kusini.
Staa huyo wa nyimbo za Nataka Kulewa, Moyo Wangu, Mbagala na nyinginezo alienda nchini humo kurekodi video ya wimbo wake mpya na pia kujiendeleza katika elimu ya masuala ya muziki.
Akizungumza na gazeti hili jana Meneja wa Diamond, Bob Tali alisema kuwa msanii huyo alikuwa nchini humo kwa takribani wiki tatu kujiendeleza kielimu katika masuala ya muziki.
Awali watu mbalimbali katika mitandao ya kijamii walionekana kukejeli ziara hiyo ya Diamond kwa hasa wakikejeli suala la kwenda kusoma kwa kuwa walisema kuwa msanii huyo alificha alichoenda kusomea nchini humo.
Akilizungumzia suala hilo Bob Tali alisema
" Najua huyu ni msanii ambae ni mmoja kati ya wasanii wakubwa wa hapa nchini na kila anachokifanya kuna watu wanaomkubali na wale ambao wanataka kumchafua tu, huyu alienda kusomea masuala ya muziki pamojana kufanya video yake kwa hiyo ni kama kozi fupi hivi."
Katika hatua nyingine Bob Tali alibainisha kuwa msanii huyo aliekuwa awasili hapa nchini jana akitokea Kenya ambapo alikuwa aunganishe ndege aliyotokanayo Afrika Kusini alishindwa kuwasili asubuhi kutokanana moto ulioripuka katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomoto Kenya nchini humo.
Akizungumzia hilo alisema kuwa wakati moto ukitokea alikuwa uwanjani hapo akisubiria kuanza kwa safari ya kuja hapa nchini.
Alisema kuwa kwa alilazimika kukaa jijini Nairobi kwa muda mrefu hadi kufikia jana jioni na ndipo aanze safari ya kuja Tanzania.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment