Kampuni
ya simu za mkononi ya Zantel imeunga mkono juhudi za kusaidia vijana
kuchangamkia fursa, kampeni inayoendeshwa pia kupitia tamasha la Fiesta.
Kampeni
hizo ni za kuhamasisha vijana kuchangamkia fursa zilizopo nchini ambapo
zitaendana na tamasha la Fiesta linaloendeshwa kwenye zaidi ya mikoa 13 kwa
kushirikiana na Clouds Media Group.
Katika
kila mkoa kampeni hiyo itakuwa ikifanyika siku moja kabla ya siku ya tamasha la
Fiesta.
Kwa
mkoa wa Kigoma alikuwepo msanii Mrisho Mpoto pamoja na Ambwene Yesaya, AY ambao
kwa pamoja walikuwa kivutio katika kuhamasisha vijana kujituma na kuwa wabunifu
katika kutumia fursa katika nyanja mbalimbali ikiwamo ya muziki.
Mada
zitakazojadiliwa kwenye semina hizo ni pamoja na ubunifu, ujasiriamali,
Uongezaji thamani kwenye bidhaa au shughuli yoyote unayofanya pamoja na kujenga
ushirikiano, uwekezaji pamoja na lugha.
Akizungumzia
semina hizo, Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan, amesema kampuni yake
imekuwa msitari wa mbele katika kuwawezesha vijana, na kwa semina hizi wanaamini
vijana wengi watapata nafasi ya kuzitambua na kujifunza.
‘Tanzania
ina fursa nyingi sana kwa vijana, na sisi Zantel tunaamini nafasi hii itakuwa
muhimu kwa vijana kujifunza na kutambua fursa zilizopo kutoka kwa wataalamu
mbalimbali’ alisema Khan.
Naye
Mkurugenzi wa Utafiti na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba,
alisema nchi ya Tanzania ina fursa nyingi lakini tatizo limekuwa ni namna ya
kuzitumia fursa hizo.
‘Tumeandaa
semina hizi kwa kutambua tatizo kubwa lilipo kwenye jamii yetu, umaskini na
ukosefu wa ajira kwa vijana, jambo ambalo semina hizi zitaenda kutatua’ alisema
Mutahaba.
Mojawapo
wa wazungumzaji kwenye semina hizo atakuwa Mrisho Mpoto, mwakilishi wa mfuko wa
hifadhi ya jamii (NSSF), Ruge Mutahaba pamoja na wageni waalikwa mbalimbali.
Kwa
mwaka huu semina hizo zimeanzia mkoa wa Kigoma, katika Ukumbi wa Kibo Hall
Park, na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya.
0 comments:
Post a Comment