WAKATI muda wa kuomba mkopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kufika mwisho, jumla ya wanafunzi 115,431 wameomba kupatiwa mikopo na bodi hiyo.
Mkurugenzi wa Mawasiliamo wa Bodi hiyo, Cosmas Mwaisobwa alisema wanafunzi 54,370 ambao ni waombaji mikopo wa mara ya kwanza waliokwishakamilisha maombi yao.
Alisema pia wanafunzi 61,061 ambao wanaoendelea na masomo yako katika vyuo vya elimu ya juu wametuma maombi ya kutaka bodi hiyo kuendelea kuwakopesha.
Wanafunzi 98,025 wa vyuo vya Elimu ya Juu nchini wanatarajiwa kupata mikopo katika mwaka wa fedha 2013/14 ambayo ni ongezeko la asilimia 2.4 ambapo Sh bilioni 306 zimetengwa kwa ajili hiyo..
Mchakato huo ulioanza Mei Mosi mwaka huu na kufikia tamati Julai 30 mwaka huu ambapo wanafunzi walitakiwa kujaza fomu za maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, aliposoma bajeti ya wizara hiyo hivi karibuni, alisema Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) itatoa mikopo kwa wanafunzi 35,649 ambao ni waombaji wapya na 62,376 wanaoendelea.
Kutokana na idadi iliyojitokeza kuomba mkopo huo iliyotolewa na HESLB kunahatari ya wanafunzi wapatao 18,721 wakakosa mkopo kutokana na bajeti iliyopo.
Waziri Kawambwa katika hotuba yake, alisema mwaka unaomalizika wa 2012/13, wanafunzi 98,773 waliwasilisha maombi na kati yao, 95,594 ndiyo waliopatiwa mikopo.
Wizara iliomba Bunge liidhinishe matumizi ya Sh bilioni 689 kwa mwaka ujao wa fedha na kati ya hizo Sh bilioni 306 ni kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi hao.
|
0 comments:
Post a Comment