Serikali
imeongeza kiwango cha alama za kuwachagua wanafunzi wanaotakiwa kwenda kujiunga
na elimu ya vyuo vya ualimu.
Awali
ilikuwa ni mhitumu wa kidato cha nne mwenye alama division 4.28 alikuwa anaweza
kujiunga na elimu ya ualimu lakini kwa sasa ni wale wenye division 4.27 tu.
Hatua hii ni
nzuri kwa kuwa inawapatia nafasi wanaojiunga na ualimu kuwa katika mazingira
mazuri ya kuwafundisha wanafunzi kwa kuwa nao wanakuwa ni wenye uelewa zaidi.
Hayo
yalisemwa leo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Shukuru Kawambwa wakati
akijibu maswali bungeni.
Tutaendelea
kuwajulisha yanayojili bungeni Dodoma katika sekta hii ya elimu ambayo ni
muhimu kabisa hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment