Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Zantel Awaichi Mawalla kulia akiwa pamoja na majaji wa EBSS 2012 wakiwa wamesimama kuomboleza msiba wa meli wa Zanzibar
Washiriki nao wakiwa wamesimama kuomboleza msiba huo
Baadae waliendeleza zoezi la kufuatilia vipaji ambapo pia walitoa elimu kwa washiriki waliojitokeza katika usaili mkoani hapo.
Na Mwandishi wa elimuboratanzania, Mbeya
WASICHANA wawili pamoja na
wavulana watatu wamechaguliwa kuuwakilisha mkoa wa Mbeya katika fainali za
taifa za shindano la kusaka vipaji la Epiq Bongo Star Search (EBSS 2012)
Washindi hao ambao kwa sasa
majina yao wala
picha zao havitakiwi kutangazwa kwenye vyombo vya habari walionesha uwezo
mkubwa katika kuimba nyimbo mbalimbali.
Akizungumzia vipaji vya Mbeya
jaji mkuu wa EBSS 2012 Ritha Paulsen alisema kuwa washindi hao wametoka katika
kundi la vijana zaidi ya 500 waliojitokeza mkoani hapa.
Alisema kuwa mbali na mkoa wa
Mbeya kusifika kwa kuimba nyimbo za injili lakini wameweza pia kuonesha uwezo
katika nyimbo nyingine mbalimbali za kidunia.
Alisema kuwa wamefanikiwa
kuwafundisha muziki vijana wengi ikiwa pamoja na kuwaelimisha juu ya namna ya
kutoka zaidi sit u kimuziki bali pia hata katika masuala mengine ya sanaa.
“ Mbali na washiriki kuja kwa
nia ya kuimba lakini pia wapo ambao wamegundulika kuwa na uwezo wa kuigiza na
kufanya aina nyingine za sanaa ambazo tumewaelekeza kuzifanya” alisema Ritha.
Alisema kuwa tofauti na mikoa
mingine katika mkoa wa Mbeya ameshuhudia akinamama wenye vipaji wakishiriki
kuimba kitu ambacho alisema kuwa ni tofauti na mikoa mingine walioenda.
0 comments:
Post a Comment