Help Children
Love them
Saidia Watoto

Thursday, July 12, 2012

TEA kuchangisha bilioni 2.3 kusaidia ujenzi wa hosteli za wasichana

 Meneja wa mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Slyivia Lupembe akifafanua jambo kwa waandishi wa habari
 Waandishi wa habari wakichukua habari ya kuhusiana na uchangiaji huo wa hosteli za wanafunzi wasichana


Kaimu Mkuu wa TEA Esther Bayo akisisitizia jambo kuhusiana na uchangiaji huo
Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA) kesho itazindua rasmi kampeni ya kuchangua ujenzi wa hosteli za wanafunzi wasichana kwa shule nane za sekondari nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TEA Esther Bayo alisema kuwa uzinduzi huo utafanyika katika wilaya ya Kibaigwa ambapo mgeni rasmi atakuwa ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi nchini Philip Mulugo.
Alisema kuwa kampeni hiyo inalenga kujenga hosteli 30 ambapo kiasi cha fedha kilicholenga ni shilingi bilioni 2.3 huku kila bweni likiwa li nagharimu milioni 78 bila samani.
Alisema kuwa ujenzi huo ukikamilika utawanufaisha wanafunzi wa kike 1,504 na kuwaepusha dhidi ya hatari mbalimbali zinazowakabili kwa sasa.
Alisema kuwa shule ambazo zitanufaika na mradi huu ni pamoja na sekondari za Ufana iliyopo Manyara, Mibukwe iliyopo Tanga, Kibaigwa iliyopo Dodoma, Milola iliyopo Lindi, Nyihara iliyopo Mara, Lundo iliyopo Ruvuma, Butundwe Mwanza na Buseko Hill iliyopo mkoani Kigoma.
Akizungumzia mikakati ya muda mrefu ya serikali katika kufanikisha ujenzi wa hosteli hizo alisema kuwa serikali inakusudia kujenga hosteli 100 katika maeneo mbalimbali nchini.
Alisema kuwa katika mpango huo mpya wa ujenzi wa hosteli hizo 100 wanafunzi 4800 watanufaika nazo na zinatarajiwa kukamilika mwaka 2015.
“ Hivyo tunaomba kuwa kila mwenye nia ya kusaidia katika hio ajitaidi kufanya hivyo kwa kuwa ndio tutawasaidia hawa wanafunzi wetu wa kike ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali” alisema Esther.
Mwisho

0 comments:

Post a Comment