Jaji Master Jay akitoa elimu kwa mmoja kati ya washiriki waliojitokeza katika usaili wa Mwanza
Mshiriki akiwa anasikilizia elimu hiyo mara baada ya kumaliza kuimba na kuambiwa kuwa alichemka.
Na Mdau wa
elimuboratanzania, Mwanza.
VIJANA wa
mkoa wa Mwanza wameelezea kufurahishwa kwao na elimu ya bure iliyotolewa na
majaji wa EBSS mkoani Mwanza ambapo waliahidi kufanyia kazi elimu hiyo.
Elimu hiyo
ni kuhusiana na namna ambavyo wanaweza kujifunza kupandisha sauti zao, kupanga
vina na kuimba aina zote za sauti.
Wakati huohuo
katika hali isiyokuwa ya kawaida wakazi wa mkoa
wa Mwanza juzi walijitokeza kwa wingi katika usaili wa shindano la Epiq Bongo
Star Search (EBSS) mkoani hapa hali iliyosababisha wengi wao kukosa nafasi ya kuimba na kulazimika kurudi tena jana.
Katika
usaili huo uliofanyikia katika uwanja wa CCM Kirumba ulihudhuriwa kwa mamia ya
wasichana na wavulana huku wengine wakiwa wamebeba vifaa mbalimbali vya muziki kuashiria kuwa
wanaifahamu vema fani hiyo.
Zoezi la
kuimba lilianza majira ya saa mbii asubuhi ambapo majaji walianza kusikiliza
vipaji hivyo na ilipofika majira ya saa kumi na moja jioni bado kulikuwa na
watu wengi waliokuwa bado wanahitaji nafasi ya kuendelea kuimba.
Kutokana na
muda kuwa umeenda walilazimika kuambiwa kurudia tena jana huku wengi baadhi yao
walikuwa wamefanya siku ya kwanza vema waliitwa tena kuimba kwa mara ya pili
ili kuchaguliwa.
Mmoja kati
ya wafanyakazi wa kampuni ya Benchmark
Production inayoandaa shindano hilo alisikika akisema kuwa hali hiyo
haijawahi kutokea kwa mkoa wa Mwanza kwa kuwa watu wamekuwa wakijitokeza kila
mwaka lakini sio kwa idadi hiyo.
Mkoa wa
Mwanza ambao mwaka juzi ulitoa mshindi wa shindano hilo Paschal Casian umekuwa
na hamasa kubwa ya wakazi wake kujitokeza kwa wingi kushiriki katika shindano
hili kubwa na la aina yake linalodhamiwa na kampuni ya simu za mkononi ya
Zantel.
poa
ReplyDelete