Help Children
Love them
Saidia Watoto

Friday, July 20, 2012

Kipindi cha kufundisha vijana maisha kimerudi tena







Na Mwandishi wa Elimuboratanzania 
SHINDANO la Maisha Plus ambalo huendeshwa kwa kuonyeshwa katika televisheni kila siku, limerudi baada ya kutofanyika kwa mwaka mmoja.


Kipindi hicho chenye kuelimisha, kuburudisha na kuhamasisha masuala mbalimbali ya maisha kipo tena hewani baada ya kukosekana kwa muda wa mwaka mmoja.\
 
Mratibu wa kipindi shindano hilo, Masoud Ali (Kipanya) amesema shindano hilo litaanza kurushwa tena mara baada ya kukamilika kwa usaili wa washiriki unaotarajia kuanzia mkoani Arusha.

Masoud amesema shindano hilo ambalo liliwahi kufanyika mara mbili, safari hii linakuja na nguvu mpya na burudani ya aina yake.

"Maisha Plus hatukuifanya mwaka jana, kuna marekebisho makubwa tumeyafanya ambayo yatalifanya hili liwe bora kuliko yaliyopita,"anasema Masoud maarufu kwa jina la Kipanya.

Ameongeza kuwa shindano hilo mwaka huu litaambatana na shindano dada la Mama Shujaa wa Chakula ambalo pia liliwahi kufanyika mwaka jana.

Katika muungano huo amesema Washiriki wa Mama Shujaa wa Chakula wataingia katika kijiji cha Maisha Plus wiki mbili kabla ya kuanza rasmi kwa shindano hilo.

"Safari hii shindano tunaliunganisha na hili la Mashujaa wa Chakula linaloandaliwa na Oxfam ambao pia ni wafadhili wetu mwaka huu," anasema Kipanya.

Safari hii shindano hilo litawakusanya vijana kutoka mikoa 14 ya Tanzania Bara na Visiwani, baadhi ya mikoa itakayoshiriki ni pamoja na Morogoro, Dodoma, Tanga, Arusha, Moshi, Mbeya, Mtwara, Dar es Salaam, Zanzibar n.k

0 comments:

Post a Comment