Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa
(kushoto), akikadidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. mil 26, Mwenyekiti wa
Kamati ya Harambee wa Taasisi ya Hasaam Maajar Trust (HMT), Dk Sinare Yusufu,
kwa ajili ya kununa madawati 745 yatakayogawiwa katika shule za msingi zilizopo
wilaya ya Njombe na Makete. Anayeshuhudia katikati ni Kaimu Meneja Mkuu wa
Tigo, Andrew Hogdson ambayo imetoa Fedha hizo zilizotokana na michange ya
matembezi ya hiari ya ‘Tigo Tuchange.’
Na Mwandishi wa Elimubora
Tigo
imekabidhi fedha zilizopatikana katika
mfuko wa matembezi ya hiari ya Tigo Tuchange kwa Hassan Maajar Trust (
HMT), ni mpango wa muda mrefu uliyoundwa
ili kuboresha mazingira ya kusoma mashuleni kwa kugawa madawati katika shule
mbalimbali za wahitaji.
Sherehe
za makabidhiano zilihudhuriwa na Mheshimiwa Dr. Shukuru Kawambwa , waziri wa elimu
na mafunzo ya ufundi stadi, wanachama wa HMT , mwandamizi mtendaji wa Tigo na
wafanyakazi.
“Moja
ya lengo letu ni kuhakikisha wanafunzi wana vifaa vya kujifunzia na mazingira
tulivu ya kusomea”alisema Mh. Dk
Kawambwa. Tunawapongeza Tigo kwa kutoa ushirikiano mzuri kwa raia na
tunaomba makampuni mengine kuisaidia serikali katika kuleta maendeleo endelevu katika nchi” hii alisema.
Hundi
ya Sh. 26, 000,000 iliwasilishwa kwa
niaba ya Tigo na Andrew Hudgson,Kaimu meneja Mkuu , kwenda kwa Mkurugenzi
mtendaji wa HMT, Zena M Tenga. Fedha zilipatikana kwa njia ya ukusanyaji wa Tigo rusha top ups iliyofanywa
mida ya saa 5 asubuhi na 12 jioni siku ya tarehe 3 March.Wateja ambao waliweka
muda wa mawasiliano kwa muda huo walitumia muda wao wa mawasiliano wakati
kuenda kiasi kama hicho kwa mpango huo
Mpango
huu ni kulingana na dhamira yetu ya
kushirikiana na jamii katika kuelewa
mahitaji ya jamii zinazotuzunguka maeneo tunayofanyia biashara, ili kutengeneza
mchango mzuri na endelevu katika kuwainua” alisema Bw.Hudson “ Tungependa
kuwashukuru tena wote kwa mchango wenu katika mfuko huu muhimu’ alisema
Chini ya mradi wa shule 5 (tano) kutoka wilaya mbili (Njombe
& Makete) zilizoko wa mkoa wa Iringa
zitapokea madawati kama ifuatavyo: Maendeleo: 135, Umoja: 196,Kumbila: 200,
Makonde: 152 na Mbela: 37.
Shule zilichaguliwa kulingana na kuwepo kwa haja kubwa
zaidi. Mradi hautafaidhisha tu shule na wanafunzi, bali kwa kununua madawati
ndani ya nchi kutasaidia katika kutengeneza nafasi za ajira kwa wafanyabiashara
na vijana katika maeneo hayo na hivyo kuleta maendeleo ya kiuchumi katika
sehemu hizo.
“Ningependa
kutoa shukrani za dhati kwa niaba ya HMT
kwenda kwa Tigo katika kushiriki kwao kuwapatia watoto hawa fursa itakayowafanya ya kuweza kujitegemea na kwa upande wa
kuwawezesha na kuwaruhusu wale kuhitaji misaada yao katika siku zijazo,” Bi.
Tenga. “ Mwanafunzi anaposoma katika mazingira mazuri na tulivu wanakuwa na
umakini zaidi na kuzalisha matokeo mazuri zaidi na hyivyo kupata maisha bora
baadaye, na kwa kupitia miradi endelevu
ya namna hii tunaweza kuleta jitihada kubwa katika kuleta maendeleo ya
uchumi ndani ya jamii, “ alisema.