Mkurugenzi wa Benchmark Production akimpokea mtoto mshiriki huyu aliyefahamika kwa jina la Joha
Mkuu wa Mawasiliano wa Zantel Awaichi Mawalla akitoa damu kuchangia kituo cha damu cha Dodoma, pia alitoa elimu na kuwasihi vijana kujitokeza kuchangia damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu wenye mahitaji ya damu
Mshiriki huyu ni mwanafunzi wa kidato cha sita na alijitaidia kuonesha uwezo wake ingawaje hakufikia kiwango na majaji walimpatia elimu ya muziki na kumtaka afanye vema
Hawa walipongezana kwa hatua waliyofikia ingawaje hawakupita lakini walinufaika na elimu ya muziki siku hiyo.
Na Mwandishi wa Elimubora Dodoma
PAZIA la shindano la Epiq
Bongo Star Search (EBSS) kwa mkoa wa Dodoma
limefungwa rasmi huku vipaji kibao vikiwa vimejitokeza na kuwavutia majaji.
Kilichovutia zaidi ni
washiriki wa miaka 16 ambao walionekana kuimba vema na kuwa kivutio hata kwa
washiriki wenzao waliofurika katika ukumbi wa Royal Village.
Akizungumzia shindano hilo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Benchmark
Production inayoandaa shindano hilo
Ritha Paulsen alisema kuwa amevutiwa na wingi wa washiriki mkoani hapa hasa
idadi ya washiriki wasichana pia.
Alisema kuwa ikiwa ni mara ya
kwanza kuruhusu washiriki wa miaka 16 kuingia katika usaili wa EBSS 2012
ameshuhudia hazina kubwa ya vipaji vya
washiriki wa umri huo.
Katika usaili huo kulikuwa na
washiriki wa aina mbalimbali wakiwamo wanafunzi, wafanyabiashara ndogondogo,
vijana wa mitaani na wadau wengineo wa muziki.
Kwa kuthamini umuhimu wa
akina mama na watoto mshiriki aliefika kuonesha kipaji chake katika ukumbi huo
alipewa nafasi ya kuimba ili aweze kuwahi kuondoka.
Naye Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano wa Zantel ambao ni wadhamini wakuu wa EBSS 2012 Awaichi Mawalla mbali na kuvutiwa na ushiriki
wa vijana waliojitokeza pia alihamasisha upimaji wa damu kwa kuchangia damu kwa
kituo cha damu mkoani Dodoma.
“ Kwa kupitia EBSS 2012
tunataka kuwafikia vijana sio tu katika muziki bali pia hata katika kuhamasisha
masuala mbalimbali yahusuyo jamii kama vile
hili la kuchangia damu na mengineo” alisema Awaichi.
Washindi watakaopatikana
watatangazwa baadae katika vyombo vya habari. Baada ya Dodoma
kwa sasa inafuata Zanzibar
ijumaa ijayo katika eneo la Ngome Kongwe.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment