Mkurugenzi Mkuu wa Economic and Social Research Foundation, Bohela Lunogelo
Mtafiti kutoka Taasisi ya Research on Poverty Alleviation (REPOA) Jamal Msami akichangia mada
Mwenyekiti wa kamati ya hesabu za serikali John Cheyo ambae pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi akizungumza na ofisa habari wa Repoa Hannah Mwandolwa
Mbunge wa Kilwa Kaskazini Murtaza Mangungu(kushoto) mtafiti kutoka Repoa Msami (katikati) na Kongi Lugola Mbunge wa CCM jimbo la Mwigora.
Na Mwandishi wa Elimu Bora
SERIKALI
imetakiwa kuvitumia vema vyanzo mbalimbali vya mapato ili kuongeza pato la
taifa kutokana na ukusanyaji wa kodi katika vyanzo hivyo.
Rai hiyo
ilitolewa juzi na mtafiti kutoka Shirika la Utafiti wa Kuondoa Umaskini (Repoa)
Jamal Msami wakati akitoa mada katika semina ihusuyo maandalizi ya bajeti iliyoshirikisha
kamati ya bunge ya hesabu za serikali.
Msami
alisema kuwa serikali inashindwa kuchangia asilimia kubwa katika bajeti yake ya
mwaka kwa kukosa fedha huku ikipoteza asilimia kubwa ya mapato kwa kushindwa
kukusanya kikamilifu kodi.
“ Serikali
inatakiwa kuhakikisha kuwa inafanya utafiti na kugundua vyanzo vipya vya mapato
ambavyo vinaweza kutozwa kodi badala ya kung’ang’ania vyanzo hivyo vilivyopo
kila siku huku bado havitoi pato la uhakika” alisema Msami.
Pia alisema
kuwa wananchi wanatakiwa kushirikishwa
kikamilifu katika upangaji wa bajeti hiyo ili kushirikisha maoni yao katika bajeti
na pia aliwataka wabunge kufuatilia upangwaji wa matumizi ya fedha katika bajeti
hiyo na kujua itakavyowanufaisha
wananchi.
Naye Mbunge
wa Kilwa Kaskazini Kongi Mangungu alitaka kuongezwa kwa muda wa kujadili bajeti hiyo kabla ya kuanza
kwa kikao cha bunge akisisitiza kuwa muda wa wiki mbili wanaopewa hautoshi.
Pia
aliishauri serikali kuweka mkakati utakaosaidia watu kutoka mikoa ya mbali
kwenda mijini kutafuta huduma za mbalimbali kwa kuwa asilimia kubwa ya mzunguko
wa hela unaamia katika miji hiyo.
Aliongeza
kuwa serikali inatakiwa kupunguza misamaha ya kodi inayotoa kwa wawekezaji kwa
kuwa inaikosesha serikali fedha ambazo zingesaidia katika bajeti yake.
Bunge la
bajeti linaanza kesho huku bajeti ya mwaka huu ikiwa ni trilioni 13 na serikali
ikiwa imechangia silimia 40 ya fedha hizo.
0 comments:
Post a Comment