Na
Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Fedha na Uchumi William Mgimwa amesema kuwa
wataalamu katika sekta ya fedha wanatakiwa kujiamini na kuwa na mikakati
endelevu kwa lengo la kukuza na kuinua uchumi wa nchi.
Mgimwa alisema hayo hivi karibuni wakati
akizingua matawi mawili ya benki ya Ecobank yaliyopo Quality Mall na Mwenge
ambapo alisifia uzinduzi wa matawi hayo mapya kwa kusisitiza kuwa huo ni
ushahidi wa kuwa na wafanyakazi wenye kujiamini na kuwa na nia na maendeleo.
Alisema kuwa iwapo wachumi wa kiafrika wakijiamini
wataiwezesha sekta binafsi kuunganisha uchumi bora kwa
manufaa ya watanzania na waafrika kiujumla.
“Kwa benki inayomilikiwa na
Waafrika, kusimamiwa na Waafrika,
kwa ajili ya kuhudumia kwa Waafrika na
wafanyabiashara wa Afrika, kukua ndani ya miaka 25 tu na kuwa
taasisi ya fedha yenye daraja la dunia na sifa za kimataifa, ni kweli
inastahili pongezi.” Alisema Mgimwa.
Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya Ecobank Tanzania Limited Peter Machunde alisema
kuwa benki hiyo tayari ina matawi matano
katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam, ina mpango wa kufungua tawi
jingine Arusha na Mwanza kabla ya mwisho wa mwaka 2012.
Alisema
kuwa benki hiyo inalenga kuboresha uchumi wa nchi kwa
kutoa bidhaa na huduma kulingana na nguvu na uongezekaji wa mahitaji ya wateja.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment