Baada ya semina walipata picha ya ukumbusho
Mratibu wa matukio wa Basata Malimi Mashiri kitoa somo
Salama akichangia mada
Somo limekolea
Madam Ritha akihitimisha semina hiyo
Na Mwandishi wa BSS
BARAZA la
Sanaa la Taifa (BASATA) limeendesha semina ya siku moja kwa majaji wa shindano
la Epic Bongo Star Search 2012 kwa kuwataka kuzingatia maadili ya kazi zao.
Akitoa somo
kwa majaji hao mratibu wa matukio wa Basata Malimi Mashili aliwataka majaji hao
kutambua kuwa asilimia kubwa ya
washiriki wanategemea zaidi msaada wao katika kukuza vipaji.
Mashili
aliwataka majaji hao kutambua kuwa mazingira waliyotoka washiriki na kuangalia
namna ya kuwasaidia kulingana na mikoa yao kwa kuwa wapo ambao wana vipaji
lakini wanatatizwa na suala la kuyazoea mazingira.
Alisema kuwa
kwa kuwa mwaka huu EBSS itaruhusu washiriki wa miaka 16 hivyo ni vema zaidi
wakazingatia suala la sauti kulingana na umri wa mshiriki sababu watakuwepo
wenye sauti za kitoto pia.
Pia
aliwataka majaji hao kuhakikisha kuwa hawatoi aina yoyote ya upendeleo na wala
kuwa karibu zaidi na baadhi ya washiriki wa shindano hilo.
Pia alisisitiza
kuwa majaji wanalo jukumu kubwa la kuwaelekeza namna ya kuimba, kuvaa,
kujiheshimu na usafi wa mwili pia.
“Hiii ni
semina ya kuwekana sawa tu kwa kuwa hili shindano lipo kwa muda mrefu na majaji
mmekuwa mkifanya vema, kwa niaba ya BASATA napenda kuchukua muda huu kuwataka
muwe makini katika kuzingatia maadili haya niliyoyasema na hata mengine
pia”alisema Mashili.
Naye
Mkurugenzi wa Berchmark Production inayoandaa shindano hilo Ritha Paulsen
alisema kuwa semina hiyo ni muhimu kwa majaji kwa kuwa muda mzuri wa kukumbushana mambo muhimu
yahusuyo muziki.
Epiq Bongo
Star Search mwaka huu inaanzia mkoani Dodoma Juni 16 katika ukumbi wa Royal
Village.
Majaji wa
shindano hilo waliohudhuria ni pamoja na Jaji Mkuu Ritha Paulsen, Master Jay,
Salama pamoja na mratibu wa EBSS kutoka
Basata Vicky Temu.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment