Na Mwandishi Wetu
MSANII wa muziki wa kizazi kipya
nchini Nasib Adbdul ‘Diamond’ anatarajiwa kupamba shindano la kumsaka Miss
dar Intercollege 2012 linalotarajiwa kufanyika Juni 22 kwenye ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa , uliopo mkabala na chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Mratibu wa shindano hilo Dina
Ismail alisema jana kwamba mbali na Diamond, onyesho hilo pia litapambwa na
burudani kutoka bendi ya Skylight iliyopo chini ya mshiriki wa Tusker
Project Fame mwaka juzi, Anneth Kushaba.
Alisema maandalizi ya shindano
hilo yanakwenda vema ambapo warembo 14 watakaosghiriki wanaendelea na
mazoezi katika hoteli ya The Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini
Dar es Salaam
“Mwaka huu tumejipanga vema
kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss Dar Intercollege anafanya vema
katika fainali za Miss Tanzania ,”alisema Dina.
Warembo watakaoshiriki shindano
hilo wanatoka vyuo vya Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ)
na Time, Ustawi wa Jamii, Usimamizi wa Fedha (IFM) na
Chuo Kikuu huria (OUT ambapo taji linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM, huku
mshindi wa pili wa mwaka jana, Blessing Ngowi alitinga fainali za Miss
Tanzania.
Dina aliwataja warembo hao kuwa
ni pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda
Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff,
Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila
Hassan.
Shindano hilo limedhaminiwa na
kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s,Dodoma Wine, Ndege
Insurance, Skylight Band,Lamada Hotel, Screen Masters,Makumbusho ya Taifa, Mustafa
Hassanali, Shear Illusions, Lamada Hotel,Grand Villa Hotel, Sporti Kizaa
zaa, Clouds Fm na blog za Michuzi, Mamapipiro, Bin Zubeiry,Mtaa kwa Mtaa na
Fullshangwe.
mwisho
|
0 comments:
Post a Comment