Help Children
Love them
Saidia Watoto

Monday, April 23, 2012

Ujamaa Art Gallery yakabidhi hundi Milioni 4 kwa UNHCR

 Baadhi ya wadau wa sanaa ya uchoraji na wafanyakazi wa UNHCR wakifuatilia tukio hilo
 Mwanafunzi wa shule ya kimataifa ya Tanganyika Tom Pado akizungumzia juu ya mchango wa klabu ya wanafunzi katika kusaidia Shirika hilo
 Wahusika kutoka Ujamaa Art Gallery (kushoto) Naibu Mwakilishi wa UNHCR Chansa Kapaya (katikati) huku kuliwa ni wahusika kutoka Shule ya Tanganyika wakiwa na Mkuu wa Shule hiyo Tom Pado
Pia Lona alikitangaza kitabu kilichoandaliwa kwa michoro ya watoto waliopo katika kambi ya wakimbizi, kitabu hicho kinauzwa kwa shilingi 20000/ ambapo watoto wameshiriki kuchora michoro mbalimbali katika kitabu hicho.

Habari Kamili.

UJAMAA Art Gallery hivi karibuni ilikabidhi milioni nne kwa ajili ya kusaidia watoto waliopo katika kambi za wakimbizi nchini kwa lengo la kuinua vipaji vyao katika uchoraji.

Akziungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi hundi ya milioni nne, Lona alisema kuwa kupitia Gallery ya Ujamaa iliyopo Mbuyuni njia ya kuelekea Mwenge, Dar es salaam iliendesha mafunzo kwa watoto waishio katika kambi ya wakimbizi ambapo watoto hao walifundishwa naman ya kuchora na kutumia rangi katika kupendezesha michoro.

Lona alisema kuwa Gallery yake iliratibu mauzo ya picha hizo ambapo ilifanikiwa kukusanya milioni nne kwa njia ya mauzo ya picha hizo.

Alisema kuwa fedha hizo zitasaidia kununua bidhaa mbalimbali za kuchorea kwa watoto hao, pia alisema kuwa wanafunzi wengi walichora picha za kuvutia zaidi na zenye kuwa na mtazamo chanya picha ambazo zimewekwa katia kitabu hicho na kinapatikana katika Gallery ya Ujamaa.

0 comments:

Post a Comment