Tigo Yadhamini Siku ya Taaluma kwa
Vyuo Vikuu
Wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali na vyuo
watapata fursa ya kujumuika pamoja katika siku ya Taaluma iliyodhaminiwa
na Tigo, na kupata fursa ya kukutana na waajiri wa makampuni mbalimbali kuanzia
saa tatu asubuhi hadi saa nane mchana katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa.
Vyuo vitakavyohudhuria ni pamoja na Taasisi ya
Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha
Ardhi, Chuo cha Ardhi, Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na vinginevyo.
Wanafunzi watakuwa na nafasi ya kufahamiana, kupata taarifa za taalum na kupata
taarifa moja kwa moja kutoka kwa waajiri ambao watakaokuwepo katika siku ya
maendeleo ya taaluma.
“Katika uchumi wa leo kuna
changamoto nyingi, makampuni lazima yavute watu wenye vipaji bora ili
kuendeleza ushindani. “Tukio hili linawasaidia waajiri kuangalia watu wenye
vipaji zaidi,” alisema Alice Maro ambaye ni Afisa Uhusiano wa Tigo. ‘’Vijana
wenye taaluma na motisha mbalimbali na wanafunzi wapya wanaweza wakajaribu
taaluma wanazozipata darasani katika mazingira halisi ya kazi (Kwa vitendo)
kwani wanaweza kuwa sehemu za hizo kampuni siku za karibuni’’ alisema.
Burudani ya moja kwa moja kutoka bendi za muziki wa
hapa nyumbani itatolewa na Mapacha Watatu na wasanii mbalimbali kutoka Chuo cha
IFM wakati wote wa tukio na baada ya hapo wanafunzi watajumuika pamoja katika
ukumbi wa Cine Club.
0 comments:
Post a Comment