Help Children
Love them
Saidia Watoto

Thursday, April 26, 2012

Alice Foundation yaandaa hafla ya michezo kwa watoto waishio katika mazingira magumu

 Kulikuwa  na mashindano ya kunywa soda kutoka kwa baadi ya watoto ikiwa ni sehemu ya kujifurahisha
 Watoto wakipata chakula cha mchana baada kucheza
 Kulikuwa na usafiri wa kuwachukua na kuwarudisha nyumbani

Baadhi ya michezo ikiwamo ya kuvuta kamba na mengine ilikuwapo ambapo pia watoto ambao ni wanafunzi katika shule mbalimbali katika kata ya Ubungo na watoto wengine pia walikutana na kubadilishana mawazo.

Habari Kamili.

Taasisi ya Alice yenye makazi yao eneo la Sinza jana iliandaa hafla kwa watoto waishio katika mazingira magumu waishio katika kata ya Ubungo ambapo pia iliwakutanisha watoto hao na wengine waliopo shuleni.

Akizungumza na Elimubora Mkurugenzi wa Alice Foundation alisema kuwa hafla hiyo inalenga kuwaweka pamoja watoto waishio katika mazingira magumu kuwafariji na kuwapati ushauri nasaha.

Alisema kuwa watoto 400 walishiriki hafla hiyo iliyoshirikisha michezo mbalimbali kama vile kuvuta kamba, mbio za mayai katika kijiko, kunywa soda, kupokezana vijiti, kukimbia na magunia.

Alisema kuwa watoto walifurahia tukio hilo na alisisitiza kuwa litakuwa likifanyika mara kwa mara.

Taasisi hiyo ya Alice inajishughulisha pia na masuala ya utunzaji wa mazingira, uwezeshaji wa akina mama, haki za wanawake, kusaidia watoto waishio mazingira magumu na  masuala ya Mkukuta.


0 comments:

Post a Comment