Hii ni barabara ya Kuu ya Wilaya ya Rungwe iliyokuwa imefungwa na wanafunzi wa sekondari ya Isongole kabla ya kubembelezwa na Polisi kuifungua
Hapwa wakiwa wamesimama katikati ya barabara hiyo kabla ya kuifungua ambapo awali waliifunga kwa saa nne kufuatia mwenzao wa kidato cha pili Nuru Patric kufariki dunia baada ya kugongwa na gari la abiria
Mkuu wa usalama wa Wilaya ya Rungwe Bl Lihwa akiwasihi wanafunzio hao kuachana na mgomo huo na kuifungua barabara hiyo mara moja.
Hoja
Vitendo kama hivyo vya wanafunzi kuamua kufunga barabara kwa maelezo kuwa wenzao wamegongwa na magari na kufariki, je ni njia sahihi au ni wapi wanapata nguvu ya kufanya maamuzi hayo mpaka kufikia hatua kuwa askari wanawabembeleza wao ili waruhusu wananchi kupita?
Ni vema wanafunzi wakatambau kuwa kuna taratibu za kisheria ambazo zinapaswa kufuatwa katika kushughulikia kila jambo na sio uamuzi wao wa kuamua kufunga barabara watakavyo.
0 comments:
Post a Comment