Ndugu Mtanzania,
YAH: NIFAHAMU
Rejea
kichwa cha habari hapo juu. Naandika kukuomba mtanzania mwenzangu kuungana na
mimi kwa kushiriki kwenye kampeni ya Nifahamu. Lengo kuu la kampeni hii
ni kuelimisha jamii kuondokana na mtazamo hasi kwa walemavu wa ngozi nchini
ambao umekuwa ukiendelea kwa miaka mingi sasa.
Mtazamo
huu umechangia kuleta maafa mbalimbali kwa walemavu wa ngozi, kwa mfano: mauaji
ya kikatili, kukatwa kwa viungo vyao na hivyo kuwaongezea ulemavu zaidi,
kutengwa na kutohusishwa kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo ya
jamii,kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni.
Walemavu
wa ngozi wanachangamoto nyingi sana katika jamii. Ukiachana na mtazamo hasi, wanakumbwa
na majanga mengi yafuatayo: hatari ya ugonjwa wa saratani ya ngozi, imani
potofu, uoni hafifu na jamii kuwa na uelewa mdogo juu ya ulemavu wa ngozi.
Nikiwa
miongoni mwa walemavu wa ngozi, nimeanzisha shirika lisilo la kiserekali (BADEF) linalohusika
na kuleta ustawi kwenye maisha ya walemavu wa ngozi nchini.
Tumezindua
kampeni hii tukiwa na ujumbe ufuatao:
a)Nilinde
– Nina haki ya kuishi kama binadamu mwingine yeyote, pia nahitaji hifadhi ya
maisha yangu.
b)Nijali – Ninastahili heshima, kuthaminiwa na
kupewa huduma na mahitaji maalumu
c)Nielimishe
– Niwezeshe kujitambua, na kujilinda na jamii initambue na kunilinda
d)Naweza
– Ninastahili kupewa fursa kama binadamu mwingine yeyote
e)Nipende
– Mimi ni mwanadamu kama mwingine yeyote na ninastahili furaha, mapenzi na
huruma.
Jamii
ya watu wenye ulemavu wa ngozi inatengwa na kunyanyasika sana. BADEF, kwa
kutambua hilo imeandaa matembezi ya hisani yenye lengo la kukusanya kiasi cha
fedha cha Tsh. Milioni 500 kwa ajili ya kuchangia ili kuboresha maisha ya watu
wenye ulemavu wa ngozi nchini kupitia njia zifuatazo:
a).Kufanya
tafiti mbalimbali juu ya hali ya watu wenye ulemavu wa ngozi kv. Kielimu,
kiafya na kijamii;
b).Kutoa elimu
ya ulemavu wa ngozi;
c).Kuhamasisha
ujumuishwaji kwenye sekta mbalimbali nchini na;
d).Kutoa vifaa
vya kukinga
0 comments:
Post a Comment