Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Nyayo Za Mama inayojishugulisha na sanaa ya uchoraji na kunakshi picha ya Nyayo Za Mama,
Candida Bahame (kulia) akimuonesha mdau wa picha Jese Mnguto picha anazoziuza
katika Gallery ya Ujamaa (Picha na Mpigapicha Wetu)
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Nyayo Za Mama inayojishugulisha na sanaa ya uchoraji na kunakshi picha ya Nyayo Za Mama,
Candida Bahame (kushoto) akipongezana na Mkurugenzi Mtendaji wa
Ujamaa Art
Gallery Lona Mashiba wakati wa ufunguzi wa maonesho ya mauzo ya kazi z sanaa za
Mama Bahame yanayoendelea katika Gallery hiyo iliyopo Mbuyuni njia ya Mwenge
(Picha na Evance Ng’ingo)
Sehemu y apicha hizo zebnye ujumbe mbalimbali wa kuelimisha
Mkurugenzi
wa Ujamaa Art Gallery Lona Mashiba akizungumza na wageni waliojitokeza wakati
wa maonesho ya picha za Candida Bahame yanaoendelea katika Ujamaa Art Gallery
iliyopo eneo la Mbuyuni njia ya kuelekea Mwenge
Mkurugenzi
Mtendaji wa Ujamaa Art
Gallery Lona Mashiba (wa kwanza) akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa Linaloshughulikia Wakimbizi (UNHCR) Chansa Kapaya wakiangaliwa
picha zilizochorwa na mchoraji Candida Bahame.
Habari Kamili
Na Mwandishi
Wetu
WANAJAMII
wametakiwa kutumia kazi za sanaa za mikono za wasanii wa hapa nchini katika
kupamba nyumba zao ili kuongeza hamasa na maendeleo ya tasnia hiyo hapa nchini.
Wito huo
ulitolewa juzi na Mdau wa sanaa za uchoraji Candida Bahame ambae ni Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Nyayo Za Mama wakati akizindua maoenesho ya wiki mbili
ya kazi zake za sanaa.
Candida
alisema kuwa wasanii wa hapa nchini wanao uwezo wa kuchora na kutengeneza picha
kwa kutumia viashiria mbalimbali vya kisanii ambavyo zinapendezesha nyumba.
Alisema kuwa
wanajamii wakiwa na utamaduni wa kununua kazi zao za sanaa na kuzipamba
majumbani kwao watakuwa kwa kiasi kikubwa wamesaidia kukua kwa sanaakiwa kama
mdau wa kazi za sanaa ya uchoraji hapa
nchini.
“ Mimi naona
kuwa muda umefika kwa hoteli zetu, ofisi na hata nyumba zetu watu kutumia picha
za wasanii wa hapa nchini katika kupamba nyumba zao ili kuonesha kuwa
wanathamini na kutambua sanaa zetu hapa nchini” alisema Candida.
Akizungumzia
sanaa yake hiyo ambayo alisema kuwa alianza tangia miaka ya 1980, Candida
alisema kuwa gharama ya picha zake anazipanga kulingana na muda aliotumia
kuzichora pamoja na umaridadi wa picha hizo.
Alisema kuwa
anatumia kipaji chake kufikisha ujumbe kwa njia ya maneno ambapo anatumia shanga
kushona maneno yenye ujumbe na pia anatumia shanga kutengenezea picha.Maonesho
hayo ya wiki mbili yanaendelea katika Ujamaa Art Gallery.
Mwisho