Muda wa kuonja embe ulikuwa ni kama hivi |
Hawa ni wadau wa shamba la Kilodede lililopo Mkuranga nao walikuwapo kuonesha bishaa zao za embe kama zinavyoonekana hapa chini |
Hili ni shamba la mwenyekitti bwana Burton Nsape |
Wadau wa shamba la Vikawe lililopo mkoa wa Pwani waliwaonjesha watu maembe yao hapohapo |
Pi amiche mbalimbali ya miembe ya kisasa ilikuwapo ikiuzwa mahala hapo |
waoneshaji walikuwapo wengi wa kutosha siku hiyo |
Vikawe wakitoa maelezo kwa wananchi walioenda kufahamu ukulima wao wa embe |
Embe ni moja kati ya mazao
mengi ya biashara ambayo yanaweza kuongeza
pato la nchi iwapo likitiliwa mkazo katika kuandaliwa na kutafutiwa soko nje ya
nchi.
Katika maonesho ya siku tatu yaliyoshirikisha
wadau kadhaa wanaohusika na embe yaliyofanyika katika uwanja wa Mnazi Mmoja
kuanzia jumamosi iliyopita hadi juzi kulikuwa na mengi ya kujifunza kuhusiana
na embe.
Katika maonesho hayo
yaliyoandaliwa na Chama cha Wakulima wa Embe nchini (Amagro) yalihusisha
wanachama zaidi ya 30 wa chama hicho
ambapo walionesha aina mbalimbali za embe ambazo zinaweza kulimwa na kutumiwa
kibiashara.
Mwenyekiti wa Amagro Burton
Nsape akizungumza kuhusiana na namna ambavyo chama chake kinawasaidia wakulima
wa embe kujipatia kipato kupitia zao hilo anasema kuwa Amagro hutoa elimu kwa
wanachama wake.
Nsape anasema kuwa wakulima
mbalimbali walikuwa wakilima na kuuza hadi nje ya nchi embe kw amuda mrefu
ambapo anafafanua kuwa ni biashara nzuri na yenye faida kubwa.
Anasema kuwa Amagro inaendeleza
harakati za kuwapatia wanachama wake elimu ya maarifa mbalimbal kuhusiana na
ukulima wa zao hilo kama vile namna ya kudhibiti wadudu waharibifu, namna ya
kufunga na kuhifadhi embe ikiwa pamoja na matumizi ya madawa na mbolea.
Anasema kuwa changamoto kubwa
inayowakabili wakulima wa embe ni ukosefu wa usafirishaji wa kitaalamu kutoka
mashambani hadi kuelekea kwenye soko kwa kuwa ili kuweza kuliweka embe katika
ubora wake kuna mengi zaidi ya kuyafuata.
0 comments:
Post a Comment