|
Waombolezaji wakiwasili kwenye msiba wa Sajuki uliopo nyumbani kwake Tabata |
|
Msanii wa filamu Tea na mdau wa filamu nchini Zamaradi wa Clouds Fm na kipindi cha Take One cha Clouds Tv |
|
Wasanii wakiomboleza kushoto ni Monalisa |
|
Dokii akiingia msibani |
|
Bibi wa Marehemu akiiingia nyumbani |
|
Sebuleni wanandugu wakiwa wanaomboleza |
|
Aha we acha tu, anaovyoonekana kusema Yusuph Mlela |
|
Wasanii hawa ndio walikuwa kwenye filamu ya mwisho ya merehemu ambayo haikutoka inaitwa Mwanasheria |
|
Wastara yani ilikuwa ni vigumu kuvumilia na kujikuta akilia muda wote kushoto ni mama wa marehemu aitwae Zaitun |
|
Sehemu ya mbele ya nyumba ya marehemu |
|
Viti na mahema vikiletwa kwa ajili ya waombolezaji |
|
Ndo Sajuki mwenyewe huyo akiwa na mkewe Wastara walipendeza sana |
Habari Kamili
Msanii mahiri wa filamu nchini Juma Mlowoko, Sajuki, amefariki dunia na anatarajiwa kuzikwa kesho katika makaburi ya Kisutu, hili ni pigo la kwanza katika tasnia ya filamu nchini kwa mwaka 2013.
Msanii huyu amefariki huku akiwa ameacha somo kubwa katiak tasnia hiyo ambalo ni uwajibikaji kwa kuwa alikuwa akiwajibika kabla na hata baada ya kuumwa kwa kuwasaidia wasanii chipukizi na hata kuisaidia tasnia nzima ya filamu kiujumla.
Uwajibikaji ndio kitu ambacho blog hii inawasihi wasanii na wadau wengine wa elimu kutambua kuwa kuwajibika ndio kunaweza kuleta mabadiliko atika kitu chochote kile.
Sajuki aliwajibika katika kuimarisha mahusiano yake na mkewe tangia kiwa mpenzi wake ambapo mkewe huyo akiwa mpenzi wake bado kwa bahati mbaya alipata ajali na kukatwa mguu lakini Sajuki alilibeba hilo na kulifanya la kwake na kuendelea kumhudumia mpenzi wake huyo hadi kufunga nae ndoa.
Poleni wanafamilia, Poleni wasanii Bwana alitoa bwana ametwaa jina lake lihimidiwe
0 comments:
Post a Comment