Steve Nyerere akataka kuhakikisha kuwa wasanii wanaandamana kama ambavyo wanavyofanya Chadema kwa kuwa kwa kufanya hivyo ndio heshima itakuja kwao |
Aisee kauli hiyo ilimkasirisha sana Mboto mpaka akataka kuhakikisha kuwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu kujiuzulu na kutaka awakome kabisa wasanii nchini |
Ahaa!! Yani huyu mwanamama ndio anatuchanganya sisi yani hata Kikwete mwenyewe anatusadia lakini huyu anatukatisha tamaa yani sisi eti hatujasoma |
Huyu alitaka kujua uwezo wa kazi wa bodi hiyo na iweje iwachanganye hivyo |
Wasanii wa tasnia ya filamu na Maigizo nchini leo wameonesha kukerwa kwao na kauli iliyokuwa ikitolewa mara kwa mara na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Joycee Fisoo kuwa hawana elimu ya kutosha.
Wasanii hao kwa pamoja wameamua kuendesha maandamano ya kutaka mama huyo aachie ngazi ili kupisha mtu anayejua sanaa na kuwatetea maslahi yao .
Wakati huohuo wasanii hao wamepinga viwango vya malipo ambavyo
vimewekwa na bodi ya filamu nchini vinavyotakiwa kulipwa na wasanii wa tasnia
hiyo.
Wasanii hao
waliokutuna juzi na jana katika ukumbi wa Vijana Social Hall kwa pamoja walionekana kupinga
viwango hivyo huku wengine wakisisitiza kuwa bodi hiyo imewasariti baada ya
kuwasaidia.
Alisema kuwa
iwapo msanii atakuwa akitaka script yake hiyo isomwe haraka haraka basi
itatakiwa alipie laki moja.
Alisema kuwa
pia iwpao mwandaaji wa filamu akitaka kutumia wasanii kutoka nchi za Afrika Mashariki atatakiwa kulipia
120,000/= huku wasanii wa kigeni wan je ya Afrika Mashariki watatakiwa kulipiwa
dola 500.
Pia alisema
kuwa kibali cha kutengeneza filamu imekuwa ni laki 5 huku kama mtayarishaji
akiwa anataka kupewa kibali kwa haraka itabidi alipie milioni moja huku kama
mtayarishaji ni mgeni kutoka nje ya nchi basi atatakiwa kulipia dola 3000.
Wakati Sangu
akisoma maelezo hayo wasanii walikuwa wakizomea huku wengine wakitoa maneno ya
kulalam akuwa viwango hivyo ni vikubwa.
Sangu
aliendelea kuwasomea wasanii hao viwango hivyo ambapo aliwataarifu kuwa
kubandika barabarani tangazo la kutangaza ni shilingi 5000 kwa tangazo moja.
Alisema kuwa
adhabu zitakazotolewa kwa watu watakaokiuka taratibu hizo watatozwa faini za
hapohapo ya milioni moja ikiwa pamoja na amri ya kusitisha utengenezaji wa
filamu hiyo.
“ Mimi naona
kuwa hii bodi inataka watu turudie hali zetu za wizi, kuzurura na tushindwe
kupata hiki kidogo tunachokipata kwa sasa, na hii ni kinyume na Rais Kikwete
atakavyo” alisema Sangu.
“ Yani kama
ukipewa kibali cha kuitengeneza filamu kwa miezi mitatu ni shilingi laki tano
lakini sasa iwpao miezi mitatu ikiisha na haujamaliza filamu yako basi itabidi
ulipie tena laki 5 nyingine sasa hii ni adhabu na itapelekea watu kutengeneza
filamu mbovu zisizokuwa na umuhimu” alisema Sangu.
Mbali na
hayo lakini pia Sangu aliendelea kuishutumu bodi hiyo huku akiendelea kutupa
lawama za wasanii hao kwa Katibu Mtendaji wa Bodi hiyo Joyce Fisoo kuwa amekuwa
akiwakejeli wasanii kuwa hawana elimu.
Kufuatia
kauli hiyo wasanii walipandwa na jazba huku wengine wakianza kutoa lawama zao
kwa katibu mtendaji huyo kuwa anatakiwa kujiudhulu.
Tunaendela na juhudi za kumtafuta mama Fisoo na tutawajaurisha muda si mrefu
0 comments:
Post a Comment