Na Katuma Masamba
MFUKO wa Pensheni
wa Watumishi wa Serikali za mitaa (LAPF)
jana umetoa msaada wa vifaa mbalimbali
vya michezo vyenye thamani ya Sh milioni 8.5 kwa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Akikabidhi msaada
huo Meneja wa LAPF kanda ya Mashariki Lulyalya Sayi alisema, wanatambua umuhimu
wa michezo nchini na hasa katika kujenga kiafya za wananchi na ndio sababu kubwa
iliyovuta kutoa vifaa hivyo ikiwa ni
seemu ya majukumu ya mfuko huo kuhudumia jamii ya Watanzania.
Alisema licha ya
kuwa na mahitaji makubwa, wameona ni vyema kutoa kile walichoweza wakiamini
kwamba itasaidia kufanikisha michezo ya mwaka huu ya Jumuiya ya michezo ya vyuo
vikuu nchini (TUSA) kwa kuwa utakidhi mahitaji muhimu hasa jezi na mipira.
“Ni muhimu
kuendeleza michezo kwani huleta nguvu na afya, na LAPF inawaomba msisite
kuendelea kuwasilisha maombi ya vifaa kama hivi vya michezo au vingine na sisi
tutasaidia kila tutakapoweza” alisema Sayi.
Aidha, aliongeza
kuwa LAPF imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia kuendeleza michezo nchini
ambapo kwa mwaka jana walitoa vifaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na vifaa vya
michezo kwa jumuiya ya michezo ya vyuo vikuu nchini (TUSA) kwa ajili ya michezo
kitaifa.
Naye Naibu Makamu
Mkuu wa Chuo hicho anayeshughulikia Mipango, Fedha na Utawala Profesa Shabani Mlacha ameishukuru LAPF kwa msaada huo ambao amesema utasaidia katika
kuendeleza michezo chuoni hapo na kuendeleza vipaji vya wanafunzi.
Msaada uliotolewa
ni pamoja na jezi jozi 27, 10 kwa ajili
ya netiboli na 17 kwa ajili ya mpira wa miguu, mipira 25, vizibao jozi 24,
soksi, glovu seti mbili pamoja na nyavu nne za mpira wa wavu .
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment