Msanii wa muziki wa kizazi kipya Barnaba akikaribishwa na Nancy Sumari |
Mabalozi wa elimu nchini Nancy Sumari (kushoto) Faraja Kota (kulia) na Rebeka Giuni (katikati) wakijadiliana jambo |
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Barnaba akiwa na mabalozi wenzake mara baada ya kujiunga nao |
Mratibu wa blog hii ya elimuboratanzania ambayo pia ni moja kati ya blog zinazodhamini Evance Ng'ingo akiwa na Barnaba |
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Shukuru Kawambwa akisalimiana na na Barnaba |
Waziri Kawambwa akifafanua jambo kuhusiana na matembezi ya hisani lakini pia alimkaribisha Barnaba katika kampeni hiyo |
Ofisa wa TEA akimpatia kipeperushi Barnaba |
Na Mwandishi wa elimuboratanzaniablog
MSANII wa muziki wa kizazi kipya Barnaba ameungana na mabalozi wengine katika kuhamasisha ujenzi wa hosteli za wanafunzi wasichana.
Barnaba anaunga na Nancy Sumari, Faraja Kota na Rebeka Giuni katika kampeni hiyo inayolenga kukusanya bilioni 2.3 na kujenga hosteli 30 ambapo Barnaba atashiriki matembezi hayo.
Habari kamili
MAMLAKA ya
Elimu Tanzania (TEA) imeandaa matembezi ya hisani ya kuchangia fedha kwa ajili
ya ujenzi wa mabweni 30 ya wanafunzi wa kike.
Matembezi hayo
yataanzia katika eneo la Mlimani City kesho kuanzia saa moja hadi saa tano
asubihi ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Uwekezaji na Uwezeshaji Mary Nagu.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Shukuru
Kawambwa alisema kuwa matembezi hayo ni moja kati ya harakati ya kuchangisha
bilioni 2.3 kwa ajaili ya ujenzi wa mabweni hayo yatakayohudumia wanafunzi wa
kike 1,504.
Alisema kuwa
mikoa ambayo inahitaji mabweni hayo kwa wingi ni Mara, Kigoma, Rukwa, Tanga,
Dodoma,Manyara, Lindi na Magu .
Alisema kuwa
ni vema wananchi wakajitokeza kwa wingi kuunga mkono juhudi za ujenzi wa mabweni
hayo kwa kununua fomu za ushiriki ambapo alisema kuwa fomu zinauzwa kwa
shilingi 20000/= katika ofisi za TEA.
“ Mimi naona
kuwa hizi ni juhudi nzuri ambazo zinafanywa na hawa watu wa TEA kwa kushirikiana
na mabalozi wetu mbalimbali na kuna
jukumu la kila mmoja wetu katika kuhakikisha kuwa wanafunzi hawa wanasaidiwa
uhakika wao wa mahala pa kulala kwa kuwajengea hizi hosteli” alisema Waziri
Kawambwa.
Lengo la
serikali ni kujenga mabweni 100 kwa lengo la kuhudumia wanafunzi wa kike 4,800
nchini ili kuwanusuru na hatari ya kupata ujauzito wakiwa shuleni.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment