Aliendesha elimu hiyo katika mazingira rafiki zaidi ambapo alicheka na kuzungumza na wanafunzi |
Hakusita pia kuonesha mikogo ya kiuanamitindo |
Wanafunzi walijaa wengi katika ukumbi wa mikutano |
Baada ya kusoma walipata nafasi ya kupiga picha za pamoja |
Furaha ilioje |
Jokate akiwa na uongozi wa |
Akiwa na watoa mada wengine na uongozi |
Wanafunzi walijikuta wakitoka nje kupiga nae picha |
Mabusu kutoka kwa wanafunzi |
Huyu sijui wanafahamiana |
Habari kamili
Mwanamitindo anaezidi kupata umaarufu kila kukicha Jokate Mwegilo alishirikiana na wanafunzi wa Tambaza wanaounda kundi la TEEN katika kuwahamaisha wanafunzi kuhusiana na masuala mbalimbali ya kijamii.
Jokate aliwasihi wanafunzi hao kujitambua na kuepuka vishawishi mbalimbali ambavyo vinaweza kuwaingiza katika tatizo la mimba na matatizo mengineo mengi.
Jokate ambae anamiliki lebo ya Kidoti alionekana kuwavutia sana wanafunzi hao ambapo waliuliza maswali mbalimbali yahusuyo elimu hyo ya kijamii.
Mtandao huu unampongeza Jokate kwa juhudi zake hizo na pia unaungana na vijana ambao wanachochea mabadiliko kama ambavyo hawa wa TEEN wanavyofanya.
0 comments:
Post a Comment