Help Children
Love them
Saidia Watoto

Tuesday, September 4, 2012

Polis wazingatie mafunzo yao kuhusiana na masuala ya haki za binadamu




Huyu askari alimwelekezea mtutu tumboni na kumsambaratisha marehemu. Ni wazi watu wa Iringa wanamfahamu askari huyu.

Kama ni kesi, askari huyu anaweza kuhojiwa. Nimekata picha kusitiri mwili wa marehemu.

Marehemu kafa akipigania haki za wanahabari, ni wakati wa wanahabari kushirikiana vinginevyo wanasiasa wataendelea kutumia vibaya vyombo vya dola dhidi yetu.


Pembeni ni shangingi la RPC, askari huyu naye kashuhudia kitendo hiki cha kikatili. Wanahabari tushirikiane kupiga kelele. Hapa walikuwa wamemaliza unyama wao wakimwondoa mwenzao aliyeumia eneo la tukio

Maiti ilisambaratishwa kabisa utumbo, si uungwana kuweka picha kama hizo hapa.
 
haya ni mabomu ya machozi
Chini ni mwili wa marehemu Daudi Mwangosi unavyoonekana baada ya kufumuliwa na risasai za askari polisi      MODS, naomba mniruhusu niweke picha zenye sura za walioshiriki kitendo hiki cha kihuni ambacho ni uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu kama kamera yangu ilivyokinasa.

Nina picha ambazo zimechukuliwa zinazoonyesha walioshiriki na jinsi walivyoshiriki. Hata RPC alikuwepo eneo la tukio.


Ujumbe kutoka blog hii
Inatakiwa waandishi pamoja na wadau wengine wa masuala ya haki za binadamu kuendelea kutoa elimu ya masuala ya haki za binadamu kwa maaskari ili waelimike zaidi

0 comments:

Post a Comment