Mkoani Dar es Salaam, wilaya ya Ilala kuna shule ya Msingi
iitwayo Kivule ambayo ina jumla ya wanafunzi 3,585; madarasa 11, waalimu 30, na
madawati 300. (Kwa mujibu wa takwimu zake za Januari 2012).
Kutokana na wingi wa wanafunzi wa shule hiyo kulinganisha na
rasilimali zake kama madawati, waalimu na madarasa; Mwalimu mkuu wa shule hiyo
Grace Ndalo alilazimika kuwagawa wanafunzi hao katika shifti mbili yaani wale
wanakuja shuleni asubuhi mpaka mchana, na wanaokuja shuleni mchana hadi jioni.
Hata hivyo, mwalimu mkuu huyo hakuishia hapo, alienda kuililia Wizara ya Elimu
na Ufundi Stadi ambao waliahidi kuongeza madarasa 7 hapo shuleni.
Mwalimu grace hakuishia hapo, alifika katika ofisi zetu na kuomba
msaada zaidi kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo. Alieleza kwamba, matatizo
makubwa mawili yanayoishambulia shule ya msingi Kivule ni:
1. ukosefu wa madawati ya kutosha (asilimia kubwa ya wanafunzi wakiwa wanakaa chini)
2. Mila potofu
zinazozunguka maeneo ya shule hiyo.
Hivyo mwalimu mkuu huyo ameomba misaada ifuatayo:
1. Madawati 895
ambapo dawati moja ni shiligi 90,000/= kwa hapa Dar es Salaam
2.
Kiasi cha fedha tasilimu
200,000/= kila mwezi kwa ajili ya kuwalipa waalimu ambao watajitolea muda wao
kuwaelimisha wazazi wa wanafunzi hao juu ya umuhimu wa elimu; pamoja na
kuwafundisha kusoma, kuandika, na kuhesabu.
Akifafanua juu ya tatizo la madawati alisema kuwa, kwa sasa dawati
moja linakaliwa na wanafunzi 5-6 (ambapo kwaida dawati moja linakaliwa na
wanafunzi 3) na bado wanafunzi wengine wanakaa chini.
Akiendelea zaidi kufafanua juu ya tatizo la pili alisema
kuwa, jamii inayoizunguka shule hiyo inaamini sana katika ndoa za mapema ambapo
wanafunzi hususani wa kike wakilazimishwa kuolewa au kupendelea kuolewa na kuoa
baada ya kutoka jandoni ama unyagoni.
Vilevile, jamii hiyo hawatambui juu ya
uzazi wa mpango, kupelekea mwanamume mmoja kuwa na hadi watoto 30 na wanawake
tofauti (hili linachangia uongezekaji wa wanafunzi shuleni hapo wakati
rasilimali ni chache). Pamoja na hayo yote, wazazi wa wanafunzi hao hawaipi
Elimu kipaumbele, hivyo msaada unahitajika kuwakomboa wazazi hao pia katika
fikra potofu ili waanze kusisitizia watoto wao umuhimu wa elimu kwani ndio
ufunguo wa maisha
.
Hasaan Majaar Trust
ingependa kushirikiana na wewe katika kuisaidia shule ya msingi Kivule.
Kitakachopatikana kitapelekwa shuleni hapo na wewe kama mfadhili wa namna moja
hadi nyingine utakuwa pamoja nasi kukabidhi rasilimali hizo.
Wasiliana nasi kupitia
·
simu
namba: +255 767 699932 / +255
718528009 / +255 685 353566 / +255 22 2775116
·
baruapepe: info@hassanmaajartrust.org
0 comments:
Post a Comment