WAHARIRI
pamoja na Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kutambua kuwa ni jukumu lao kuinua
kipato chao na hakuna mtu mwingine mwenye jukumu hilo.
Wito huo
ulitolewa juzi na Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini
(MOAT) Reginard Mengi katika viwanja vya
Karimjee wakati akizindua Chama cha Kuweka na Kukopa cha Wahariri, Wahariri
Development Saccos.
Mengi
alisema kuwa iwpao wahariri wakijiendeleza kimaisha wanaweza kuwa huru katika
kufanya maamuzi yao wenyewe kulingana na maadili ya kazi zao bila kurubuniwa na
watu wengine.
Alisema kuwa
Saccos ni njia mojawapo ya kuinua kipato chao hivyo aliwataka kuitumia vema kwa
kuchukua mikopo yenye malengo ya kibiashara na ambayo wanaweza kuirudisha kwa
muda unaotakiwa.
Pia aliwataka
kuepuka migogoro ambayo inaweza kujitokeza kutokana na saccos hiyo huku
akiwataka waitumie kama chombo cha
ukombozi wa maisha yao kwa kuimarisha wazo lao la biashara kabla ya kuchukua
mkopo.
“ Kwanza
ningependa muelewe kuwa pesa haina sura, hapa nikiwa na maana kuwa katika
kuitafuta hakuna kuwa na mzaha nayo hakuna suala la aibu wala suala la kuogopa
kuisaka” alisema Mengi.
“Natambua
kuwa mtu huwezi kuwa mhariri mzuri huku ukikabiliwa na na shida
mbalimbali, sasa basi msikubali kuishia
kupewa tu sifa kuwa nyinyi ni wahariri wazuri huku mkiwa mnakabiliwa na shida
mbalimbali” aliongeza Mengi.
Aliahidi
kuisaidia Saccos hiyo kwa kila hali ili iweze kutimiza ndoto yake na aliwaomba
wahariri kukutana nae punde watakapokuwa wanahitaji msaada wake.
Naye Mwenyekiti wa saccos hiyo Godfrey Shogolo
alisema kuwa saccos hiyo ambayo ni kwa ajili ya wahariri inalenga kuinua maisha
ya wahariri hao na kuongeza kuwa mchango wa kujiunga nayo ni shilingi 400,000/=
Uzinduzi huo
ulihudhuriwa na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.
0 comments:
Post a Comment