Viti 30 maalum kwa watoto
wenye ulemavu vimetolewa kwa watoto wenye ulemavu Zanzibar leo. Viti hivyo vimeagizwana kampuni
ya Uchimbaji na utafiti wa Madini ya Montero yenye makazi yake Canada na
washirika wake wa Tanzania Kampuni ya madini ya Wigu Hill. Viti hivi
vimetengenezwa maalum kwa ajili ya watoto walemavu na shirika lisilo la
kiserikali ‘’Wheel chairs for Kids “
huko Australia.
“Tunafurahia kuweza kupanua wigu wa misaada yetu kwa watoto
kwenye kisiwa cha Zanzibar, kama
sehemu yetu ya kusaidia jamii. Hivi viti vya matairi mawili vitaboresha maisha yao na ya wazazi na walezi wao. Siku ya leo
inaweka historia ya mkakati ambao, baadae viti vya walemavu vingine 130
vitasambazwa kwa watoto wa mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro’’alisema Grant
Pierce Meneja Mkuu wa Montero Tanzania.
Utoaji wa viti hivyo
ulifanyika rasmi katika hospitali ya Mnazi mmoja kwa ushirikiano wa klabu ya
Rotary Zanzibar ambayo ilitafuta wapokeaji na kuandaa tukio hilo.
‘’Rotary inajihusisha na
mipango mbalimbali ya kijamii huku Zanzibar
na ni wazi kwamba watoto wenye ulemavu wanamahitaji zaidi kulio vikundi vingine
vyote katika jamii yetu. Hii ni siku ya furaha tele kwao na kwetu.”Alisema
mwanachama wa RotaryStephi Said.
Viti hivi vya walemavu
vimetengenezwa kwa ustadi zaidi na vinaweza kutosheleza mahitaji ya kila mtoto
kulingana na ulemavu wake.
Kuhusu kampuni ya madini ya Montero
Kampuni ya uchimbaji wana
utafiti ya madini ya Montero ni kampuni inayojihusisha na uchimbaji wa madini
ya Rare Earth Elements (REE) na inaendesha shughuli za Mkoa wa Morogoro kupitia
washirika wake wa Wigu Hill. Pia ina maeno mengine Tanzania,Afrika
Kusini na Quebec Canada
Kuhusu Wheelchairs for Kids
Klabu ya Rotary huko
Australia Magharibi ilianzisha mkakati wa wheelchairs for kids mwaka1998,viti
hivi maalum vinatengenezwa na wafanyakazi wastaafu wanaojitolea. Mpaka sasa ina
nguvukazi ya watu wapatao 100, wengi wakiwa wastaafu, wanotengeneza,wanaohakiki
viwango,na kupanga na kupakia kwenye maboksi, viti hivi.Wafanyakazi wengine wa
kujitolea wanatengeneza foronya na zawadi ndogo ndogo zinazoambatanishwa na viti hivi, kwa ajili ya wapokeaji.
|
0 comments:
Post a Comment