Sunday, September 30, 2012
Monday, September 24, 2012
Vijana hawa wameandaliwa na kufundishwa vema na nido wanatumia elimu hiyo katika kubiridisha kwa sarakasi
8:25 AM
No comments
Wasanii wa Kikundi cha Shada, wakifanya onyesho la sarakasi katika
ufunguzi wa tamasha la kimataifa la Sanaa Bagamoyo. Tamasha hilo
limefunguuliwa rasmi Jumatatu na litaendelea kwa siku tano hadi Jumamosi
ijayo
Moja kati ya mambo yaliyokuwa kivutio kikubwa ni jinsi watoto hao walivyoonyesha umahiri katika kuruka kwenye maringi.
Wasanii wa kundi la Jeshi wakifanya onyesho la Mzingaombwe katika Tamasha la Sanaa la Bagamoyo
Sunday, September 23, 2012
Uzembe unavyoweza sababisha ajali za barabarani
6:06 AM
No comments
Tela la Roli hili lilikutwa limepinduka katika barabara ya Tabata Relini hii inatokana na uzembe wa kutozingatia elimu ya usalama wa barabarani
Hapa ni nyuma ya tela hilo
Hapa ni nyuma ya tela hilo
Thursday, September 20, 2012
MCHANGO WAKO UNAHITAJIKA HMT KUSAIDIA SHULE YA MSINGI YA KIVULE
7:23 AM
No comments
Mkoani Dar es Salaam, wilaya ya Ilala kuna shule ya Msingi
iitwayo Kivule ambayo ina jumla ya wanafunzi 3,585; madarasa 11, waalimu 30, na
madawati 300. (Kwa mujibu wa takwimu zake za Januari 2012).
Kutokana na wingi wa wanafunzi wa shule hiyo kulinganisha na
rasilimali zake kama madawati, waalimu na madarasa; Mwalimu mkuu wa shule hiyo
Grace Ndalo alilazimika kuwagawa wanafunzi hao katika shifti mbili yaani wale
wanakuja shuleni asubuhi mpaka mchana, na wanaokuja shuleni mchana hadi jioni.
Hata hivyo, mwalimu mkuu huyo hakuishia hapo, alienda kuililia Wizara ya Elimu
na Ufundi Stadi ambao waliahidi kuongeza madarasa 7 hapo shuleni.
Mwalimu grace hakuishia hapo, alifika katika ofisi zetu na kuomba
msaada zaidi kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo. Alieleza kwamba, matatizo
makubwa mawili yanayoishambulia shule ya msingi Kivule ni:
1. ukosefu wa madawati ya kutosha (asilimia kubwa ya wanafunzi wakiwa wanakaa chini)
2. Mila potofu
zinazozunguka maeneo ya shule hiyo.
Hivyo mwalimu mkuu huyo ameomba misaada ifuatayo:
1. Madawati 895
ambapo dawati moja ni shiligi 90,000/= kwa hapa Dar es Salaam
2.
Kiasi cha fedha tasilimu
200,000/= kila mwezi kwa ajili ya kuwalipa waalimu ambao watajitolea muda wao
kuwaelimisha wazazi wa wanafunzi hao juu ya umuhimu wa elimu; pamoja na
kuwafundisha kusoma, kuandika, na kuhesabu.
Akifafanua juu ya tatizo la madawati alisema kuwa, kwa sasa dawati
moja linakaliwa na wanafunzi 5-6 (ambapo kwaida dawati moja linakaliwa na
wanafunzi 3) na bado wanafunzi wengine wanakaa chini.
Akiendelea zaidi kufafanua juu ya tatizo la pili alisema
kuwa, jamii inayoizunguka shule hiyo inaamini sana katika ndoa za mapema ambapo
wanafunzi hususani wa kike wakilazimishwa kuolewa au kupendelea kuolewa na kuoa
baada ya kutoka jandoni ama unyagoni.
Vilevile, jamii hiyo hawatambui juu ya
uzazi wa mpango, kupelekea mwanamume mmoja kuwa na hadi watoto 30 na wanawake
tofauti (hili linachangia uongezekaji wa wanafunzi shuleni hapo wakati
rasilimali ni chache). Pamoja na hayo yote, wazazi wa wanafunzi hao hawaipi
Elimu kipaumbele, hivyo msaada unahitajika kuwakomboa wazazi hao pia katika
fikra potofu ili waanze kusisitizia watoto wao umuhimu wa elimu kwani ndio
ufunguo wa maisha
.
Hasaan Majaar Trust
ingependa kushirikiana na wewe katika kuisaidia shule ya msingi Kivule.
Kitakachopatikana kitapelekwa shuleni hapo na wewe kama mfadhili wa namna moja
hadi nyingine utakuwa pamoja nasi kukabidhi rasilimali hizo.
Wasiliana nasi kupitia
·
simu
namba: +255 767 699932 / +255
718528009 / +255 685 353566 / +255 22 2775116
·
baruapepe: info@hassanmaajartrust.org
wanafunzi wa darasa la saba na mitihani
6:33 AM
No comments
Wanafunzi wa darsa la saba wamemaliza mitihani yao hii leo huku wengine wakiwa wamefanya mtihani huo wakiwa katika hali mbaya ya kimsaada kwa kuwa wlaikuwa hawana hata penseli au peni za kufanyia mtihani huo.
Tuesday, September 18, 2012
Mengi atoa somo la biashara kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini
7:56 AM
No comments
WAHARIRI
pamoja na Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kutambua kuwa ni jukumu lao kuinua
kipato chao na hakuna mtu mwingine mwenye jukumu hilo.
Wito huo
ulitolewa juzi na Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini
(MOAT) Reginard Mengi katika viwanja vya
Karimjee wakati akizindua Chama cha Kuweka na Kukopa cha Wahariri, Wahariri
Development Saccos.
Mengi
alisema kuwa iwpao wahariri wakijiendeleza kimaisha wanaweza kuwa huru katika
kufanya maamuzi yao wenyewe kulingana na maadili ya kazi zao bila kurubuniwa na
watu wengine.
Alisema kuwa
Saccos ni njia mojawapo ya kuinua kipato chao hivyo aliwataka kuitumia vema kwa
kuchukua mikopo yenye malengo ya kibiashara na ambayo wanaweza kuirudisha kwa
muda unaotakiwa.
Pia aliwataka
kuepuka migogoro ambayo inaweza kujitokeza kutokana na saccos hiyo huku
akiwataka waitumie kama chombo cha
ukombozi wa maisha yao kwa kuimarisha wazo lao la biashara kabla ya kuchukua
mkopo.
“ Kwanza
ningependa muelewe kuwa pesa haina sura, hapa nikiwa na maana kuwa katika
kuitafuta hakuna kuwa na mzaha nayo hakuna suala la aibu wala suala la kuogopa
kuisaka” alisema Mengi.
“Natambua
kuwa mtu huwezi kuwa mhariri mzuri huku ukikabiliwa na na shida
mbalimbali, sasa basi msikubali kuishia
kupewa tu sifa kuwa nyinyi ni wahariri wazuri huku mkiwa mnakabiliwa na shida
mbalimbali” aliongeza Mengi.
Aliahidi
kuisaidia Saccos hiyo kwa kila hali ili iweze kutimiza ndoto yake na aliwaomba
wahariri kukutana nae punde watakapokuwa wanahitaji msaada wake.
Naye Mwenyekiti wa saccos hiyo Godfrey Shogolo
alisema kuwa saccos hiyo ambayo ni kwa ajili ya wahariri inalenga kuinua maisha
ya wahariri hao na kuongeza kuwa mchango wa kujiunga nayo ni shilingi 400,000/=
Uzinduzi huo
ulihudhuriwa na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Sunday, September 16, 2012
Mazingira ambayo yahitaji na pia yanaihathiri elimu nchini
10:52 PM
No comments
Pasipokuwa na elimu ya kutosha kwa waendesha bodaboda hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwa usalama wao kwa kuwa wengi wao watazidi kufa siku hadi siku.
Ay afanya ziara ya kimafunzo katika ofisi za magazeti ya serikali ya Habari leo na Daily news
6:34 AM
No comments
Saturday, September 15, 2012
Zantel kuwaendeleza kielimu wachezaji wa African Lyon
5:46 AM
No comments
Mmoja kati ya maofisa wa Zantel, Natasha, akitoa zawadi kwa washiriki waliohudhuria hafla hiyo
Wednesday, September 12, 2012
Wakufunzi wa makocha wapewa somo
4:25 AM
No comments
Wakufunzi wa makocha waliopo hapa jijini kwa semina ya siku nne wakipewa somo na mwalimu wao katika viwanja vya Karume jana
Mamis kinondoni wazidi kujifua, wapewa elimu ya kujiamini
4:22 AM
No comments
Mwandaaji wa Miss Kinondoni Vivian Sirikwa akiwafunda washiriki wa shindano hilo ambalo litafanyika Ijumaa hii katika ukumbi wa Kasa uliopo Mikocheni
Monday, September 10, 2012
Rais Kikwete azindua chuo cha kijeshi nchini kilichopo Kunduchi Dar es salaam
10:55 AM
No comments
Rais Jakay Kikwete akipena mkono nma Meja Jenrali Charles Makalala mara baada ya kumkabidhi funguo ikiwa ni inshara ya ufunguzi wa chuo hicho kilichopom Kunduchi, Dar es salaam |
Rais Kikwete akiwa na wakuu mbalimbali wa chuo hicho mara baada ya kukizindua leo |
Hapa akikizindua rasmi chuo hicho jana ambapo alittoa wito kuwa kinatakiwa kuendeleza elimu ya kijeshi na kuwa mfano wa kuigwa ndani na nje ya bara la Afrika |
Sunday, September 9, 2012
Msaada huu kwa watoto wenye ulemavu utawasaidia kusoma vema
6:43 AM
No comments
wheelchairs znz Ally Sihaji and son Hilali Silaji 13 years old |
Salama Zaharani (10) na wazazi wake |
Sadra Hassan (9) |
Saturday, September 8, 2012
Wanafunzi washiriki mashindano ya riadha ya taifa
5:23 AM
No comments
Friday, September 7, 2012
Elimu ya michezo ikitolewa mapema inasaidia kujenga na kuinua vipaji
7:46 AM
No comments
Watoto hawa walikutwa wakijifunza kucheza mchezo wa Tennis, mafunzo kama haya yanapotolewa mapema yanasaidia kuwajengea uwezo na kujua vipaji vyao mapema.
Ni vema wazazi wakawa wanawapeleka watoto wao katika viwanja kama hivi kujifunza michezo mbalimbali
Ni vema wazazi wakawa wanawapeleka watoto wao katika viwanja kama hivi kujifunza michezo mbalimbali
Tuesday, September 4, 2012
Mengi ya kujifunza katika maonesho ya siku ya wakandarasi Mlimani City
5:03 AM
No comments