Help Children
Love them
Saidia Watoto

Sunday, September 8, 2013

Shule ya wasichana ya Mtakatifu Christina yashinda shindano la Kiingereza



SHULE ya wasichana ya St.Christina imekuwa kinara kati ya sekondari 22 zilizoshiriki
mashindano ya kuzungumza lugha ya Kiingereza ya ‘Bavaria Malt English
Competition for Tanga secondary schools 2013’ yaliyojumuisha wanafunzi zaidi ya
100 kutoka wilaya tano za mkoani humo.

Shule hiyo ilizawadiwa seti moja ya Compyuta na printa ambapo mshindi wa pili
sekondari ya Popatlal iliondoka na seti ya Kompyuta huku Sekondari ya Rosmin
iliyoibuka mshindi wa tatu ikijinyakulia Luninga yenye ukubwa wa inch 40.

Mashindano hayo ya siku mbili yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Regal
Naivera na Mkwakwani kwa  udhamini wa
Bavaria Holland kupitia Kampuni ya Jovet (T) Limited inayosambaza kinywaji
baridi cha Bavaria Malt yalilenga kuhamasisha wanafunzi ili waone umuhimu wa
kuzungumza lugha hiyo.

Akizungumza katika hotuba ya kufunga mashindano hayo na baadae kuwatunuku vyeti na zawadi
washiriki na washindi watatu Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia masuala ya
Elimu mkoani Tanga, Ramadhani Chomola alisema mashindano hayo pamoja na
kuwawezesha wanafunzi kutambua uwezo wao pia yamewapa mwamko mpya wa kuzungumza
lugha hiyo.

“Nazipongeza shule na wanafunzi wote walioshiriki mashindano ya mwaka huu wito wangu
nawataka waongeze ubunifu na bidii ya kuzungumza Kiingereza popote wanapokuwa
ili waweze kujijenga na kwa wale walioshinda leo wasijiamini sana na kuridhika
bali wachukulie mafanikio hayo kama hatua ya kuendeleza harakati za kuwasiliana
kwa kutumia lugha hiyo ya kimataifa”,alisema.

Awali akizungumza kwenye hafla hiyo Meneja wa Uendelezaji Masoko wa BavariaHolland, Roger
ter Horst alisema kampuni hiyo inaamini kwamba ni jambo jema kusaidia jamii
kufikia malengo yake ya kupata maendeleo yake ya kiuchum na kijamii.

“Mashindano haya tumeyaasisi kwa mara ya kwanza hapa Tanga ili kurudisha shukrani kwa jamii
inayotumia bidhaa zetu tumeanza kwa kuangalia hawa vijana walioko shuleni kwa
kuwapa fursa hii ya mashindano inayowawezesha kujipa muda zaidi wa kuzungumza
Kiingereza ambayo ni miongoni mwa lugha muhimu inayotumika kwenye masomo yao na
kuwasiliana ki kimataifa”, alisema.

Nao baadhi ya wanafunzi walioshiriki wakiwemo Radhia Abubakar wa St. Christina na Sammy
Madundo wa
Popatlal aliyejinyakulia zawadi ya kompyuta ndogo (Laptop) kutokana na umahiri
na juhudi binafsi aliyoonesha kwenye mashindano hayo alisema yamempa changamoto
inayomsukuma kuongeza juhudi katika kujifunza lugha hiyo.

“Kiukweli lugha ya kiingereza sio rahisi kamlugha nyingine hii inamhitaji mtu kujifunza kwa bidii na kuizungumza wakati
wote ndipo ataweza kuwa na misamiati mingi ya kumwezesha kuitumia kwa ufasaha
binafsi pamoja na wenzangu wanne tuliowakilisha shule yetu ilitugharimu muda
mwingi wa ziada kujifunza mambo mbalimbali yaliyomo kwenye lugha hii”, alisema
Radhia.

Mashindanohayo yanatarajiwa kuendelea mwakani kwa kujumuisha sekondari nyingi zaidi
kutoka katika wilaya zote nane zenye halmashauri 11 zinazounda mkoa wa Tanga.


0 comments:

Post a Comment